NINI WAMESEMA BAADA MECHI: MOURINHO v MOYES!
>>MOURINHO: “WALIANZA VYEMA KUPITA SISI….TUNA MUUAJI KWENYE BOKSI!”
>>MOYES: “HATUKUSTAHILI BAO 2-0 NYUMA HAFTAIMU..YA VIDIC SI NYEKUNDU!”
MARA
baada ya Chelsea kuichapa Manchester United Bao 3-1 Uwanjani Stamford
Bridge kwa Hetitriki ya Samuel Eto’o, Mameneja wa Klabu hizo mbili
walihojiwa na kujibu ifuatavyo:
-JOSE MOURINHO:
"Nadhani huu ni ushindi mkubwa na
tumestahili, ndio. Jinsi nilivyokuwa nikichambua Gemu ilikuwa ngumu kwao
kuwa nyuma 2-0. Walianza vyema kupita sisi, walikuwa juu. Kipindi cha
Pili kilikuwa tofauti. Kwa Dakika 25-30 tulitawala lakini wakaja juu.
Nadhani hii gemu iko tofauti na nyingine. Kawaida tunatawala hatufungi
lakini leo shuti la kwanza tumefunga. Goli la pili lilikuwa ni la Muuaji
kwenye boksi ambae namjua Miaka mingi na inaonekana kama Samuel Eto'o
anarudi tena.”
-Kuhusu Ubingwa kwa Man United, Mourinho alisema:
“Ni ngumu, wako Pinti 14 nyuma ya Arsenal, 13 nyuma ya Man City na 12
nyuma yetu. Labda Timu moja itasambaratika lakini si zote Tatu, ni
ngumu, kwao nadhani sasa ni kupigania kumaliza 4 bora. Watafanya hivyo
kwani ni Klabu yenye fahari na utamaduni na watapigana na kushinda dhidi
ya wapinzani wengine kwa vile hatuchezi nao tena.”
-DAVID MOYES:
"Hatukustahili kuwa nyuma Bao 2-0
Haftaimu. Tulikuwa na bahati mbaya kwa Bao la Kwanza lakini yale mawili
mengine tujilaumu wenyewe. Hatukujihami vizuri na hatukupata nafasi kama
Chelsea kufunga. Tulicheza vizuri baadhi ya gemu. Tulicheza vizuri
mwanzoni, tulishindwa tu umaliziaji. Hatukufunga kwenye boksi lao,
tulishindwa kujihami boksi letu. Nadhani tulicheza vizuri katikati,
hatukufanya vyema sehemu muhimu. Hatukati tamaa, tutaendelea na
kuboresha kila sehemu, mie na Klabu tutafanya hilo.”
-Kuhusu Kadi Nyekundu kwa Vidic na Kadi ya Njano kwa Rafael, Moyes alisema:
"Sikuiona ya Rafa lakini niliona ya
Vidic. Ya Vidic si Nyekundu ni Njano. Kama ya Rafa ni mbaya basi
nitakuwa mkweli na kujitokeza kusema hilo.”