STAMFORD BRIDGE: MAN UNITED YAPIGWA 3-1, UBINGWA….BAI BAI??
>>HETITRIKI YA GWIJI WA CAMEROUN, ETO’O, YAIUA UNITED!
MATOKEO
Jumapili Januari 19
Swansea 1 Tottenham 3
Chelsea 3 Man United 1
++++++++++++++++++++++
MABINGWA
Manchester United walitawala Kipindi cha Kwanza na kujikuta wako nyuma
kwa Bao 2-0 dhidi ya Chelsea, Bao zote zikifungwa na Gwiji wa Cameroun
Samuel Eto’o, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford
Bridge waliyomaliza kwa kipigo cha Bao 3-1 ambacho kwa Wadau wao huenda
kimehakikisha kwamba hawawezi tena kutetea Taji lao kwani sasa wako
Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal huku zimebaki Mechi 16.
Pengine kilichobaki kwao sasa ni kuwania
kumaliza ndani ya 4 bora ili wafuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu
ujao kwani wapo Pointi 6 tu nyuma ya Nafasi hiyo ya 4.
Chelsea walipata Bao lao la kwanza
katika Dakika ya 17, bila kutegemewa kwani Man United ndio waliokuwa juu
kimchezo, baada ya uzembe wa kutomkaba Samuel Eto'o ambae alipokea
Mpira wa kurushwa na kumhadaa kirahisi Phil Jones kisha kupiga Shuti la
Mita 20 na kumbabatiza Mchael Carrick na kumpoteza Kipa De Gea.
Bao la Pili lilifungwa kwenye Dakika ya
45 na Eto’o kufuatia ulinzi duni baada Kona kupigwa na kuokolewa na
Mpira kumkuta Ramires aliempasia Cahill aliemsogezea Eto’o na kupachika
kilaini.
Bao la 3 lilipigwa tena na Eto’o, ni
Hetitriki kwake, kufuatia Kona ya Dakika ya 49 iliyounganishwa na Cahill
na kuokolewa na De Gea na kutua miguuni mwa Eto’o ambae alimalizia
kilaini kwa mara nyingine.
Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliifungia
Bao lao pekee Man United katika Dakika ya 78 kufuatia kazi njema ya
Danny Welbeck kumfikia Phil Jones ambae shuti lake lilionekana kutokuwa
na madhara hadi alipochomoza Chicharito.
Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada Nahodha wao Nemanja Vidic kupewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya kwa Eden Hazard.
VIKOSI:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian, Oscar, Hazard, Eto'o
Akiba: Cole, Lampard, Torres, Mata, Mikel, Matic, Schwarzer.
MAN UNITED: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra, Jones, Carrick, Valencia, Januzaj, Young, Welbeck
Akiba: Giggs, Smalling, Lindegaard, Hernandez, Cleverley, Fletcher, Kagawa.
REFA: PHIL DOWD
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
22 |
24 |
51 |
2 |
Man City |
22 |
38 |
50 |
3 |
Chelsea |
22 |
23 |
49 |
4 |
Liverpool |
22 |
25 |
43 |
5 |
Tottenham |
22 |
3 |
43 |
6 |
Everton |
21 |
15 |
41 |
7 |
Man Utd |
22 |
9 |
37 |
8 |
Newcastle |
22 |
4 |
36 |
9 |
Southampton |
22 |
4 |
31 |
10 |
Aston Villa |
22 |
-7 |
24 |
11 |
Hull |
22 |
-6 |
23 |
12 |
Norwich |
22 |
-17 |
23 |
13 |
Stoke |
22 |
-14 |
22 |
14 |
West Brom |
21 |
-5 |
21 |
15 |
Swansea |
22 |
-6 |
21 |
16 |
Crystal Palace |
22 |
-17 |
20 |
17 |
Fulham |
22 |
-26 |
19 |
18 |
West Ham |
22 |
-11 |
18 |
19 |
Sunderland |
22 |
-15 |
18 |
20 |
Cardiff |
22 |
-21 |
18 |
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatatu Januari 20
2300 West Brom v Everton
Jumanne Januari 28
2245 Man Utd v Cardiff
2245 Norwich v Newcastle
2245 Southampton v Arsenal
2245 Swansea v Fulham
2300 Crystal Palace v Hull
2300 Liverpool v Everton
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City