Header Ads

CITY KUBEBA CAPITAL ONE CUP KUTAISAIDIA UNITED KUCHEZA EUROPA LIGI!

JUMAPILI Manchester City walitwaa Capital One Cup baada ya kuifunga Sunderland Bao 3-1 naMAN_CITY-BINGWA_COC2014hivyo kufuzu kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao.
Lakini kwa vile wanategemewa sana kumaliza katika 4 Bora za Ligi Kuu England na hivyo kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI, nafasi yao ya kucheza EUROPA LIGI itakwenda kwenye Timu itakayomaliza Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England.
++++++++++++++++++++++++++++
NANI HUCHEZA ULAYA:
-Timu 4 za Juu kwenye Ligi Kuu England hucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI
-England inazo Nafasi 3 za kucheza EUROPA LIGI: Bingwa wa FA CUP, Bingwa wa Capital One Cup na Timu ya 5 kwenye Ligi Kuu England.
-Ikiwa Mshindi wa FA CUP amefuzu UEFA CHAMPIONZ LIGI, Nafasi yake kucheza EUROPA LIGI itachukuliwa na Mshindi wa Pili wa Kombe hilo.
-Ikiwa Mshindi wa Pili wa FA CUP nae amefuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI, basi Nafasi yake kwenye EUROPA LIGI itachukuliwa na Timu itakayomaliza Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu England.
++++++++++++++++++++++++++++
Msimu huu Manchester United wamekuwa wakisuasua na wapo Nafasi ya 7 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Timu iliyo Nafasi ya 4 kwenye Ligi, Nafasi ambayo ndiyo ya mwisho kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Pia wapo Pointi 8 nyuma ya Tottenham ambao wako Nafasi ya 5 ambayo ndio Nafasi ya kucheza EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
28
30
63
2
Liverpool
28
38
59
3
Arsenal
28
24
59
4
Man City
26
42
57
5
Tottenham
28
4
53
6
Everton
27
11
48
7
Man Utd
27
12
45
8
Newcastle
28
-2
43
9
Southampton
29
1
39
++++++++++++++++++++++++++++
Lakini huenda pia Timu ya Nafasi ya 7 nayo ikaweza kucheza EUROPA LIGI ikiwa Mshindi wa FA CUP nae yupo kwenye 4 Bora na hivyo kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Ikiwa Man United watafuzu kucheza EUROPA LIGI kwa kumaliza Nafasi ya 7 hilo nalo litawaletea hali ngumu kwani watalazimika kuanzia Mashindano hayo Raundi ya Tatu ya Mchujo inayoanza kuchezwa Julai 31.
Powered by Blogger.