Header Ads

Kesi ya Ekelege kuendelea leo

kwa ufupi
Awali, akimsomea hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Janeth Machulya alidai kuwa, Machi 28, 2008 mshtakiwa kwa nia ovu alitumia madaraka yake vibaya kwa kuziondolea kampuni hizo ada Dola za Marekani 42,543 (Sh68 milioni).0
ShaDar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi Mkurugenzi   Mkuu wa zamani wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege hadi leo.
Katika kesi hiyo, Ekelege anakabiliwa na mashtaka mawili, kutumia madaraka vibaya kwa kuziondolea asilimia 50 ya ada ya utawala Kampuni za Jaffar Mohamed Ali na Quality Motors.
Kesi hiyo ilitakiwa kuendelea jana, lakini iliahirishwa hadi leo na mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi.
Awali, akimsomea hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Janeth Machulya alidai kuwa, Machi 28, 2008 mshtakiwa kwa nia ovu alitumia madaraka yake vibaya kwa kuziondolea kampuni hizo ada Dola za Marekani 42,543 (Sh68 milioni).
Machulya alidai mshtakiwa aliziondolea ada kampuni hizo bila idhini ya Baraza la Utendaji, hatua ambayo ni kinyume na utaratibu wa TBS.
Shtaka la pili, ni kusababisha hasara ya Dola za Marekani 42,543. Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.
Powered by Blogger.