ANGALIA PICHA BINTI WA MIAKA 16 AELEZEA MAMBO MZITO KUHUSU FREEMASON
Binti Fauzia akiwa amepozi nyumbani kwao maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.
Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya Freemason, Uwazi linakudondoshea.
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.
Akizungumza
na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa nyumbani kwa baba
yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.
Alikuja
Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari hii ilikuwa
amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa.
Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.
ALIKOTOKEA
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza
hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye
alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama na Kigogo jijini Dar es
Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku na kufanya mambo ya
kichawi kwa watu mbalimbali.
Alisema
siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, naye kwa uwezo
aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa kwa kuugua ghafla.
Baada
ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee mmoja
(alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia
alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya
kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.
Akiendelea kuzungumza huku akionekana kujiamini licha ya umri wake mdogo, Fauzia alisema:
“Siku nilipoondoka kwenda Nigeria
nilikuwa na wenzangu walionisindikiza. Ilikuwa ni safari ya kimiujiza.
Tulipofika kule, wao waliniacha mahali, mimi nikajikuta nikitokea ndani
ya jengo kubwa ambalo ndani yake nilikuta mtu mwenye asili ya Kiarabu.
“Yule mtu alinipokea na kuishi naye. Siku moja aliniambia Fauzia wewe una na nguvu mbili, za Freemason na uchawi,” alisema.
ASIMIKWA KUWA MALKIA MDOGO
Aliendelea kusema: “Ndipo siku moja
ikafika, nikasimikwa kuwa malkia mdogo kwa kukabidhiwa gauni fupi jeupe
na kitambaa cheupe cha kuvaa kichwani (vilioneshwa kwa waandishi wa
habari hii).
Hizi nguo ni dalili kwamba anayemiliki ni malkia mdogo. Unakuwa na uwezo wa kujua mambo yote ya siri ya kidunia yanayoendelea.
“Baada
ya hapo, nilirejea hapa nchini kwetu. Nilipokewa na bibi ambaye
alikuja kimazingara. Bibi aliniuliza ni wapi nilikokuwa mpaka nimepata
nguvu za Freemason wakati yeye alinikabidhi uchawi wa kawaida?
Sikumjibu,” alisema Fauzia mbele ya baba yake mdogo na mama yake mdogo
aliyekuwa amuue.
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa
pia na majirani, binti huyo akakumbuka jambo zito lililomtokea akiwa
darasa la saba na kusema:
“Nakumbuka
nikiwa darasa la saba, siku moja usiku niliota ndoto. Nilimwona mzee
mmoja mwenye mapembe akinijia na kunikabidhi mikoba. Naamini yule mtu
ndiyo aliniingiza kwenye Freemason kwani kuanzia pale ndipo
nilipobadilika na kuwa na uwezo wa kuja Dar na kurudi Kahama kwa usiku
moja.
“Basi,
baada ya kurudi nyumbani Kahama, siku moja nikaambiwa na wakubwa wangu
natakiwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kuongeza nguvu za
Freemason.
“Kule
nilikaa kwa siku kadhaa na nikafundishwa mambo mengi ya ajabu, pia
nilikutana na viongozi wakubwa wa kidini na kiserikali wa hapa nchini
Tanzania (aliwataja majina).
MAISHA YA NYUMBANI AKIWA SAFARINI
“Ilivyokuwa ni kwamba, kila nilipokuwa
safarini, nyumbani nilikuwa naacha jini lililofanana na mimi kwa kila
kitu. Jini hilo lilifanya kazi nyumbani badala yangu pasipo mtu yeyote
kufahamu wakijua ni mimi. Niliporudi na jini liliondoka.
ATOBOA SIRI ZA SCREEN TOUCH
“Nikiwa katika jengo la ajabu la
Freemason nchini Marekani, niliona watu wengi wakitengeneza simu za
kisasa ‘screen touch’ na televisheni za ‘flat screen’ nilipowauliza za
nini? Walinijibu kuwa simu hizo zimewekwa kifaa maalumu cha kunyonya
damu ya mtumiaji kutoka kwenye kidole chake kila mara atakapobofya.
“Zamani
kulikuwa na simu zikitumia peni maalum kwenye screen lakini Freemason
waliamua kuziondoa kwa kuwa hazikuwa zikiwapelekea damu. Hivyo mtumiaji
wa simu za screen touch za sasa lazima aguse kwa kidole chake na si kwa
kitu kingine ndipo ataweza kutumia simu yake ilimradi tu achangie damu
yake kwenye benki za damu za Freemason zilizopo Marekani.”
KUHUSU TV FLAT SCREEN
Akifafanua kuhusu runinga za flat
screen, Fauzia alisema kuwa, hizo zimewekewa kifaa chenye mionzi ya
ki-Freemason ambacho humfanya mtu anayeangalia kila wakati kuwa zezeta
huku vifo vya ghafla akivitaja kama matokeo makuu ya kuangalia
televisheni hizo.
Mbali na hayo, binti huyo alizizungumzia suruali maarufu za wasichana zinazotambulika kwa jina la ‘skin tight’ ambazo hubana.
Alisema
suruali hizo zimewekwa nyuzi maalum za kijini ambazo husababisha
mwanaume yeyote ambaye atamuona msichana akiwa katika vazi hilo amtamani
kingono hata kama msichana huyo havutii.
PASAKA NA X-MASS
Binti huyo alizidi kutia hofu watu pale
aliposema kuwa Sikukuu za Pasaka na X-Mass zimekuwa kubwa duniani kwa
sababu Freemason wametia mkono kwa kuzikuza na kutumbukiza akilini mwa
watu tabia ya dhambi.
“Wengi
wanaziona sikukuu hizo ndiyo za kufanyia maasi, kama vile ngono, ulevi
kupitiliza na kufuru nyingine na wanaopotezewa uhai kwa ajili ya sikukuu
hizo ni wengi sana,” alisema.
KUHUSU KUMUUA MAMA YAKE MDOGO
Kuhusu jaribio la kumuua mama yake
mdogo, Fauzia alisema alishindwa mara zote kwa kuwa alikuwa ‘mzito’.
Aliwataarifu Freemason wenzake wamuue lakini nao walishindwa na kudai
kuwa alikuwa akiwaka moto.
Alidai
kuwa mama mdogo huyo hakujua lolote lililokuwa likiendelea mpaka pale
alipofika mpwa wao ambaye ni mlokole na kumuombea Fauzia.
MJOMBA MTU AZUNGUMZA
Akizungumza na waandishi wetu, mjomba wa
Fauzia aliyejitambulisha kwa jina la Gervas ambaye ni mlokole, alisema
kuwa kila mara alipokuwa akimuangalia binti huyo, alihisi ana mambo
tofauti na binadamu wengine.
Alisema:
“Siku moja nilimsikia roho wa Mungu akiniongoza kufika nyumbani hapa na
kuomba. Nilijikuta nikimuita Fauzia na kuanza kumuombea.
“Nilishangaa
sana kumwona akipandisha mashetani na kuzungumza mambo ya kutisha
aliyodai kuyafanya kwa siri. Baada ya maombi ya muda mrefu nikisaidiwa
na familia yangu ndipo nilipovitoa vifaa vya ajabu.”
Akizungumza na waandishi wetu, baba
mdogo wa Fauzia aliyejitambulisha kwa jina la Amos Deda ambaye anaishi
na binti huyo Kigogo na ambaye mke wake ndiyo alikuwa auawe, alisema:
“Sikuwa nikiamini kabisa kuhusiana na
masuala haya mpaka nilipojionea mwenyewe vifaa hivi vya kichawi vya
Freemason vikitolewa na mjomba wake.
“Fauzia
ameniomba msamaha, pia ameomba msamaha kwa familia. Lakini pia akasema
ajali iliyomvunja miguu shangazi yake miaka ya nyuma na kumuua mtoto wa
shangazi yake huyo aliisababisha yeye, pia akaomba msamaha. Tumeupokea.”
Pia
Fauzia aliiomba radhi kwa familia ya mama yake mdogo ambapo alidai
kumuua mama huyo kwa kushirikiana na mkubwa wake mwingine.
NENO LA MWISHO
“Kwa sasa nimeokoka, nimeachana kabisa na mambo haya, zaidi ninamtumikia Mungu kwa nguvu zangu zote,” alisema Fauzia.
-UWAZI