BIGI MECHI LIVERPOOL v CHELSEA, MVUTO MAN UNITED v NORWICH..NI CLASS OF ‘92!
>JE MOURINHO KUPANGA KIKOSI 'DHAIFU' ANFIELD JUMAPILI??
LIGI KUU ENGLAND inaelekea patamu wakati Liverpool wakikaribia kutwaa Ubingwa wao wakwanza
tangu 1990 lakini kikwazo ni Bigi Mechi ya Jumapili huko Anfield ambako
Jose Mourinho atatua na Chelsea yake wakiwa na matumaini finyu ya
Ubingwa huku macho ya Wadau, hasa wa Manchester United, wakielekeza Old
Trafford ambako Jumamosi wataikabili Norwich City wakiwa na Meneja mpya,
Ryan Giggs, akiwa na Wataalam wenzake alioanza nao tangu Utotoni, ‘THE
CLASS OF ‘92’, kina Phil Neville, Nicky Butt na Paul Scholes.
PATA DONDOO FUPI ZA MECHI ZA WIKIENDI:
+++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi 26 Aprili 2014
1445 Southampton v Everton
1700 Fulham v Hull
1700 Stoke v Tottenham
1700 Swansea v Aston Villa
1700 West Brom v West Ham
1930 Man United v Norwich
Jumapili 27 Aprili 2014
1400 Sunderland v Cardiff
1605 Liverpool v Chelsea
1810 Crystal Palace v Man City
+++++++++++++++++++++++
SOUTHAMPTON v EVERTON
-St Mary’s
Kikosi cha Roberto Martinez,
kinachowania kumaliza 4 Bora, kinaelekea Ugenini huko kwa Mtakatifu
Maria baada ya Bosi huyo wa Everton kumteketeza Bosi wa zamani wa
Everton, David Moyes kwa kumchapa 2-0 huko Goodison Park na hiyo kuwa
Mechi ya mwisho ya Moyes kama Meneja wa Manchester United.
Wakati Everton wana ushindi wa Mechi 3 mfululizo za Ugenini, Sourhampton wao hajwashinda katika Mechi zao 3 zilizopita.
FULHAM v HULL CITY
-Craven Cottage
Bosi wa Fulham, Felix Magath,
amesisitiza Timu yake haitoshuka Daraja ikiwa itashinda Mechi zake 2 za
Nyumbani zilizobaki na hii ni mojawapo.
Hull City wapo Wembley, kwenye Fainali
ya FA CUP dhidi ya Arsenal, lakini kwenye Ligi wako kipindi kigumu baada
kufungwa Mechi 4 kati ya 6 zilizopita za Ugenini.
STOKE CITY v TOTTENHAM HOTSPUR
-Britannia Stadium
Stoke City wapo kwenye wimbi zuri ambalo
wamefungwa Mechi 1 tu katika 8 zilizopita lakini Tottenham, chini ya
Meneja Tim Sherwood, hawatabiriki.
SWANSEA CITY v ASTON VILLA
-Liberty Stadium
Wikiendi iliyopita, Swansea waliifunga
Newcastle Ugenini na Straika wao, Wilfried Bony, kufunga Bao zote mbili
huko St James’ Park lakini Bony hajafunga Bao Uwanjani kwao Liberty
Stadium tangu Februari.
Meneja wa Aston Villa, Paul Lambert,
anaamini ushindi kwenye Mechi 1 kati ya 4 zilizobaki utawahakikishia
kubaki Ligi Kuu England.
WEST BROMWICH ALBION v WEST HAM UNITED
-The Hawthorns
West Brom wako Pointi 3 juu ya ya zile
Timu 3 za Mkiani ambazo hushushwa Daraja mwishoni mwa Msimu na ushindi
dhidi ya West Ham, ambao wamefungwa Mechi 3 mfululizo, utawasogeza
kwenye usalama hasa ukizingatia Mechi zao 2 zijazo ni ngumu ambazo ni
dhidi ya Arsenal, inayowania 4 Bora, na Sunderland wanaopigania uhai
wao.
MANCHESTER UNITED v NORWICH CITY
-Old Trafford
Hii
ni Mechi ya kwanza kwa Meneja mpya, Ryan Giggs, ambae kwenye Benchi
lake atakuwa nao Wachezaji wenzake wa zamani alioanza nao kuchezea Man
United tangu wakiwa na Miaka 12, kina Paul Scholes, Nicky Butt na Phil
Neville.
Hii ni Mechi yenye mvuto sana, hasa kwa
Wadau wa Man United, lakini ni Mechi ya ‘kufa kupona’ kwa Norwich City
ambao wako Pointi 2 tu juu ya zile Timu 3 za Mkiani ambazo hushushwa
Daraja mwishoni mwa Msimu.
JUMAPILI Aprili 27
LIVERPOOL v CHELSEA
-Anfield
Hii ni BIGI MECHI.
Lakini baada ya Chelsea kufungwa 2-1 na
Sunderland Wikiendi iliyopita na kuondoa matumaini yao kutwaa Ubingwa na
kufuatia wao kupata Sare ya 0-0 Ugenini na Atletico Madrid kwenye Mechi
ya Kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Juzi Jumanne, mkazo kwa Chelsea ni
Ulaya na si England tena hasa kwa kuwa wanarudiana na Atletico Jumatano
ijayo huko Stamford Bridge.
Hali hii imemfanya Jose Mourinho aombe
ridhaa ya Uongozi wa Juu Chelsea kuchezesha Kikosi hafifu dhidi ya
Liverpool ili kuwalinda Mastaa wao kwa Marudiano na Atletico Madrid na
hasa kuwachezesha Wachezaji ambao Jumatano hawatacheza Mechi hiyo ya
Ulaya.
Miongoni mwa hao ni Frank Lampard na
John Mikel Obi ambao hawezi kucheza na Atletico baada ya kuzoa Kadi za
Njano na hivyo kufungiwa kutocheza Mechi hiyo.
Pia, Chelsea haiwezi kuwatumia Nemanja Matic na Mohamed Salah kwenye Mechi na Atletico kwa vile hawaruhusiwi kucheza na UEFA.
Hivyo, Mourinho yuko huru kuwachezesha
Lampard, Obi, Matic na Salah kwenye Mechi na Liverpool bila kuathiri
mipango yake ya Gemu na Atletico.
Hata hivyo, Mourinho hawezi kumtumia
Ramires ambae amefungiwa Mechi 4 za Ligi baada kukiri kosa la kumpiga
Larsson wa Sunderland Wiki iliyopita tukio ambalo Refa Mike Dean
hakuliona na Leo hii FA kumpata na hatia.
Liverpool, chini ya Brendan Rodgers
ambae alikuwa Kocha wa Vijana na Timu ya Rizevu ya Chelsea wakati
Mourinho ni Meneja wa Chelsea katika Kipindi chake cha kwanza kati ya
2004 na 2009, wanahitaji hata Sare kwenye Mechi hii na Liverpool ili
wawe mstarini kutwaa Ubingwa lakini hadi sasa wameshashinda Mechi 11
mfululizo za Ligi.
Mourinho, ambae tayari ameshawananga
Liverpool kwa kuwaita ‘Wafalme wa Penati’, huenda asikubali kufungwa na
Liverpool na kushusha Kikosi thabiti.
SUNDERLAND v CARDIFF CITY
-Stadium of Light
Sunderlana, baada ya kuichapa Chelsea na
kutoka Sare na Man City katika Mechi zao mbili zilizopita, sasa
wanakutana na Klabu kama wao, Cardiff City, ambao wanasaka ushindi kwa
Udi na Uvumba ili wabaki Ligi Kuu England.
Sunderland wako mkiani na juu yao ni
Fulham na kufuatia Cardiff City wenye Pointi 1 zaidi ya Sunderland ambao
wana Mechi 1 mkononi.
Hii ni Fainali kwa Timu zote mbili.
CRYSTAL PALACE v MANCHESTER CITY
-Selhurst Park
Wakati Mechi hii inaanza, Man City watakuwa tayari wanajijua wamesimama wapi baada ya Liverpool na Chelsea kumaliza kucheza.
Palace wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa
kwenye wimbi kubwa la ushindi wa Mechi 5 mfululizo na City wataingia
wakiwakosa Wachezaji muhimu akiwemo Majeruhi Yaya Toure huku David Silva
na Sergio Aguero wakiwa na maamuivu nahamna uhakika kama watacheza.
ARSENAL v NEWCASTLE UNITED
-Emirates Stadium
Aaron Ramsey amerudi dimbani baada
kupona na Lukas Podolski amepiga Bao 5 katika Mechi 5 zilizopita na
Arsenal wamerudi tena kwenye Reli wakiwania 4 Bora.
Newcastle wao wametandikwa Mechi 5
mfululizo lakini safari hii Meneja wao, Alan Pardew, atakuwepo Benchi
baada kumaliza Mechi 5 za Kifungo chake.
LIGI KUU ENGLAND:
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Liverpool |
35 |
25 |
5 |
5 |
96 |
44 |
52 |
80 |
2 |
Chelsea |
35 |
23 |
6 |
6 |
67 |
26 |
41 |
75 |
3 |
Man City |
34 |
23 |
5 |
6 |
91 |
35 |
56 |
74 |
4 |
Arsenal |
35 |
21 |
7 |
7 |
62 |
41 |
21 |
70 |
5 |
Everton |
35 |
20 |
9 |
6 |
57 |
34 |
23 |
69 |
6 |
Tottenham |
35 |
19 |
6 |
10 |
51 |
49 |
2 |
63 |
7 |
Man United |
34 |
17 |
6 |
11 |
56 |
40 |
16 |
57 |
8 |
Southampton |
35 |
13 |
10 |
12 |
50 |
45 |
5 |
49 |
9 |
Newcastle |
35 |
14 |
4 |
17 |
39 |
54 |
-15 |
46 |
10 |
Stoke |
35 |
11 |
11 |
13 |
39 |
49 |
-10 |
44 |
11 |
Crystal Palace |
35 |
13 |
4 |
18 |
28 |
41 |
-13 |
43 |
12 |
West Ham |
35 |
10 |
7 |
18 |
38 |
48 |
-10 |
37 |
13 |
Swansea |
35 |
9 |
9 |
17 |
47 |
51 |
-4 |
36 |
14 |
Hull |
34 |
10 |
6 |
18 |
34 |
43 |
-9 |
36 |
15 |
Aston Villa |
34 |
9 |
8 |
17 |
35 |
49 |
-14 |
35 |
16 |
West Brom |
34 |
6 |
15 |
13 |
41 |
54 |
-13 |
33 |
17 |
Norwich |
35 |
8 |
8 |
19 |
28 |
56 |
-28 |
32 |
18 |
Cardiff |
35 |
7 |
9 |
19 |
31 |
65 |
-34 |
30 |
19 |
Fulham |
35 |
9 |
3 |
23 |
35 |
77 |
-42 |
30 |
20 |
Sunderland |
34 |
7 |
8 |
19 |
33 |
57 |
-24 |
29 |
+++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumatatu 28 Aprili 2014
2200 Arsenal v Newcastle
Jumamosi 3 Mei 2014
1445 West Ham v Tottenham
1700 Aston Villa v Hull
1700 Man Utd v Sunderland
1700 Newcastle v Cardiff
1700 Stoke v Fulham
1700 Swansea v Southampton
1930 Everton v Man City
Jumapili 4 Mei 2014
1530 Arsenal v West Brom
1800 Chelsea v Norwich
Jumatatu 5 Mei 2014
2200 Crystal Palace v Liverpool
Jumanne 6 Mei 2014
2145 Man Utd v Hull
Jumatano 7 Mei 2014
2145 Man City v Aston Villa
2145 Sunderland v West Brom
Jumapili 11 Mei 2014
[Mechi zote Saa 1700]
Cardiff v Chelsea
Fulham v Crystal Palace
Hull v Everton
Liverpool v Newcastle
Man City v West Ham
Norwich v Arsenal
Southampton v Man Utd
Sunderland v Swansea
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Stoke