Mume amuua mke akihofia siri kufichuliwa
Harusi ya wawili hao ilikuwa harusi ya kupangwa
Jasvir Ginday
Nyumba walimokuwa wanaishi Ginday na marehemu mkewe
Mwanamume mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa benki nchini Uingereza, amefungwa maisha jela kwa kumuua mke wake.
Jasvir
Ginday aliambia mahakama kuwa alimuua mkewe baada ya kumtishia kuwa
angewaambia wazazi wao kuwa mume wake hushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Jasvir Ram Ginday, mwenye umri wa miaka 29, alimshambulia mareemu mkewe Varkha Rani kwa chuma ya mashine ya kusafisha nyumba.
Mahakama ilisikia Ginday alivyomnyonga mkewe na kisha kuchoma mwili wake.
Jaji John
Warner alisema kuwa Ginday alikuwa na wakati mgumu kama mwanamume
anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja hasa kwa kuwa aliishi katika jamii
ya watu wasiokua kama yeye.
Kesi hii ilisikikilizwa kwa wiki tatu.
Harusi ya wawili hao ilifanyika baada ya Ginday kuja London kutoka nchini India kukutana na mkewe katika harusi yao ya kupangwa.
Lakini
alikuwa amemwambia rafiki yake mwaka 2008 kuwa yeye huvutiwa zaidi na
wanaume licha ya kwamba alikuwa anamuoa mchumba wake Varkha aliyekuwa na
miaka 24.
Polisi
waliambia mahakama kuwa Ginday alizoea kuzuru baa za watu wanaoshiriki
mapenzi ya jinsia moja na kwamba alizoea sana kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na wanaume wengi.
Wakati
kesi ilipokuwa ikiendelea, Ginday alidai kuwa mkewe alitishia kufichua
kwa familia zao kuwa aliozwa mwanamume ambaye hushiriki mapenzi ya
jinsia moja baada ya kupata picha chafu kwenye simu yake.
Aliambia
mahakama kuwa baada ya mkewe kupata picha hizo alikimbia chumbani na
kumtishia na hapo ndipo alipomgonga na chuma kichwani na kumuua kutokana
na hasira.
Aliwadangaya
wazazi wake kuwa mkewe alimuacha lakini baada ya uchunguzi kufanywa
polisi walipata fuvu la kichwa katika nyumba yao.(MM)
CHANZO:BBC