Rais Kikwete apewa tuzo Washington DC
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumatano jioni alipewa tuzo la kiongozi
mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika. Tuzo hilo lilipokelewa kwa niaba
yake na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw. Bernard Membe.
Sherehe
za kutoa tuzo hilo ziliandaliwa na jarida la African Leadership Magazine
Group kwenye hoteli ya St. Regis ya Washington DC.
Akizungumza
na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kutoka hoteli hiyo,
mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya Tanzania Bw. Salva Rweyamamu
alisema rais Kikwete alituzwa kutokana na huduma zake kwa jamii ya
Tanzania, lakini pia ametambuliwa kwa kuwa mstari wa mbele kutatua
migogoro barani Afrika.
Mahojiano na Salva Rweyemamu
Hotuba na sherehe wakati wa hafla hiyo zilipepereshwa hewani moja kwa moja kupitia mtandao wa mawasiliano ya internet.
Tuzo hilo
la heshima hutolewa kwa viongozi wa bara la Afrika wanaotoa mchango
mkubwa zaidi kwa jamii zao ikiwa ni pamoja na utawala bora.(MM)
CHANZO:VOA