TASAF na washirika wa maendeleo wanaofadhili Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi watembelea kisiwani Zanzibar
Mkuu
wa Mkoa wa Kusimni Unguja.Dkt. Idris Muslim Hijja, akizungumza na Ujumbe
wa Tasaf na Wawakilishi wa kutoka Nchi Wafadhi wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Masikini PSSN kabla ya kutembelea Shehia ya Kikungwi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF mwenye suti nyeusi Ndg. Ladisilaus Mwamanga,
akizungumza katika Ofisi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt Idris
Muslim Hijja, kabla ya kuaza kwa ziara hiyo.
Mwakilishi
kutoka Benki ya Dunia Bi. Ida Manjoro, akizungumza wakati walipofika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kujitambulisha kwake kabla ya
kuanza kwa ziara yao kutembelea Kaya Masikini Unguja.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Ndg. Ladisilaus Mwamanga, akizungumza na Walengwa wa
Kaya Maskini katika shehia ya Kikungwi Unguja.
Walengwa
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shehia ya Kikungwi Wilaya
yaKati Unguja wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf akizungumza
katika mkutano huo.
Picha ya pamoja
======= ===== =======
Ujumbe kutoka Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii TASAF na washirika wa maendeleo wanaofadhili Mpango wa
kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi uko kisiwani Zanzibar kuona namna
Mpango huo unavyotekelezwa kisiwani humo. Ujumbe huo umepata fursa ya
kutembelea shehia ya Kijini Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja na Shehia ya
Kikungwi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja ambako umezungumza na walengwa
wa mpango huo.
Wakizungumza na viongozi hao
baadhi ya walengwa wameonyesha kuridhika na mpango wa kunusuru kaya masikini
ambapo wamesema maisha ya kaya hizo yameanza kuboreshwa huku mmoja wa walimu wa
shule ya msingi Kikungwi Amrani Kombo akibainisha kuwa tangu kuanza kwa Mpango
huo mwaka jana kumekuwa na mahudhurio
mazuri kwa wanafunzi kutoka katika kaya masikini ikilinganishwa na hali
ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa mpango huo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema Mpango huo umeanza kutekelezwa kwa
awamu nchini baada ya serikali kuridhia utekelezaji wake katika jitihada za
kupambana na umasikini miongoni mwa wananchi. Amesema utafiti umefanywa kwa kina kuona namna ya
kuutekeleza mpango huo ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika ya maisha ya wananchi wanajumuishwa katika mpango huo.