UZINDUZI WIKI YA CHANJO YAIBUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA AFYA MAKETE
Katibu
tawala wilaya ya Makete Joseph Chota ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Makete, akitoa hotuba kwa
wananchi wa kijiji cha Isapulano
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Makete Dkt. Michael Gulaka akitoa
taarifa ya chanjo kwa mgeni rasmi na wananchi waliofika Isapulano.
Mgeni rasmi akihutubia
Mgeni rasmi Joseph Chota akitoa chanjo kwa mtoto Sarafine Mahenge.
Mgeni rasmi akitoa chanjo kwa mtoto Horence Luvanda
Mgeni rasmi Joseph Chota akitoa chanjo kwa mtoto Elifata Tweve.
Kulia ni baba aliyeonesha mfano kwa kumleta mtoto wake wa kike kupata chanjo
Wananchi wakipanga foleni kwenda kuwapa watoto wao chanjo.
==============
Ubovu
wa miundombinu ya barabara wakati wa masika katika wilaya ya Makete
mkoani Njombe umeelezwa kuwa miongoni mwa vitu vinavyochangia huduma ya
chanjo kutofika kwa wakati katika zahanati zinazotoa chanjo wilayani
hapo.
Hayo
yameebainishwa na Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Makete Dkt.
Michael Gulaka hii leo wakati akisoma taarifa ya idaya ya afya siku ya
uzinduzi wa wiki ya chanjo iliyoadhimishwa kiwilaya katika Kata ya
Isapulano wilayani Makete. Dkt Gulaka ametaja changamoto nyingine ni
pamoja na zahanati za Utengule, Ugabwa na Igolwa bado hazitoi huduma ya
chanjo kutokana na uchache wa wahudumu wa afya na upungufu wa wahudumu
katika sekta ya afya.
"Unakuta
zahanati inamtumishi mmoja hivyo anapokwenda likizo au kwenye mafunzo
huduma za chanjo hazitolewi hivyo kuathiri kufikia kiwango
kilichokusudiwa lakini si hilo tu wkati wa masika zahanati nyingi
hazifikishiwi chanjo kwa wakati kutokana na ubovu wa barabara, magari
hayafiki na wakati mwingine yanafika kwa tabu" amesema Dkt. Gulaka.
Akihutubia
wanakijiji waliofika katika uzinduzi hao Mgeni rasmi katika uzinduzi
huo Katibu tawala wilaya Bw. Joseph Chota kwa niaba ya mkuu wa wilaya
amesema serikali imejipanga vilivyo kuimarisha huduma ya mkoba kwa
maeneo yaliyombali na vituo vya kutolea huduma za afya, pamoja na
kuendelea kuomba vibali vya kuajiri watumishi wapya wa afya kama njia
mojawapo ya kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Bw.
Chota amesisitiza wazazi na walezi kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto
wao kupatiwa chanjo kwa wale ambao hawajakamilisha ili kupunguza
magonjwa ambayo yanazuilika kwa watoto.
Katika
hatua nyingine amesema kwa wilaya ya Makete kumekuwa na mwamko wa
wanaume wengi kuamua wao wenyewe kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya
afya kupatiwa chanjo tofauti na ilivyokuwa mwanzoni kuwa hilo ni jukumu
la wanawake tu, na kusema kwa kufanya hivyo kutapelekea ushirikiano wa
pamoja katika kumtunza mtoto wao.
Mgeni
rasmi baada ya kuzindua wiki ya chanjo kiwilaya ambayo imeanza leo
Aprili 24 - 30, pia ametoa chanjo kwa watoto watatu ambao ni Sarafine
Mahenge, Horence Luvanda, na Elifata Tweve kama ishara ya uzinduzi rasmi
na baada ya hapo wahudumu wa afya kuendelea kutoa chanjo kwa watoto
wengine waliofika kwa ajili ya huduma hiyo
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Chanjo ni jukumu la wote"
Picha/Habari Edwin Moshi wa globu ya jamii kanda ya nyanda za juu kusini