Header Ads

UEFA CHAMPIONS LIGI: FAINALI, NI MABINGWA BAYERN AU REAL WANAOSAKA ‘DECIMA’?


PATA TATHMINI/VIKOSI VINAVYOTARAJIWA/DONDOO MUHIMU:
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
UEFA CHAMPIONZ LIGI
NUSU FAINALI:
Marudiano
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Aprili 29
Bayern Munich v Real Madrid [0-1]
Jumatano Aprili 30
Chelsea v Atletico Madrid [0-0]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
FC Bayern Munich v Real Madrid CF
-Allianz Arena, Munich, Germany
HILI ni pambano kali sana na Mabingwa Watetezi, Bayern Munich, chni ya Meneja wao Pep Guardiola, ambae anaifahamu fika Real Madrid tangu enzi zake akiwa na Barcelona, ana kazi nzito ya kugeuza kipigo cha Bao 1-0 ili watinge Fainali.
Kihistoria, Bayern Munich wana Rekodi nzuri sana dhidi ya Real Madrid wakiwa kwao huko Munich lakini kwenye Mechi hizi Historia huwa inabaki Vitabuni tu na kuandikwa baada ya Mechi.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-Rekodi ya Bayern Munich wakiwa Nyumbani kwao dhidi ya Real Madrid ni Ushindi: 8, Sare: 1 Kufungwa: 0.
-Real Madrid wameshinda mara 2 tu katika safari zao 27 Nchini Germany, mojawapo ikiwa ni ushindi wa Bao 6-1 dhidi ya FC Schalke katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Msimu huu.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
UCL-NUSU_FAINALI-MARUDIANOAkiongelea pambano hili, Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amedai wao hawatajihami kulinda ushindi wao wa Bao 1-0 bali watashambulia kwa kutumia Mtu Tatu, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale ili kusonga Fainali na kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya ambalo wenyewe wamelibatiza Jina ‘DECIMA’
Lakini, kwa Misimu mitatu sasa, Real Madrid wamekuwa wakiishia kwenye Nusu Fainali na Msimu uliopita walibwagwa na Borussia Dortmund kwa Jumla ya Bao 4-3 kwa Mechi mbili na ule wa nyuma yake, 2011/12, walitolewa kwa Penati na Bayern Munich baada kufungana Jumla ya Bao 3-3 kwa Mechi mbili.
Safari hii Bao la Karim Benzema la Mechi ya Kwanza ndio linawatenganisha na, ukiondoa vipigo walivyopata Bayern Munich Uwanjani kwao Allianz Arena walipofungwa na Manchester City na Arsenal, hakuna Timu nyingine iliyoshinda hapo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu Msimu uliopita.
Lakini Ancelotti amesisitiza: “Ninamwamini kila Mchezaji wangu! Plani yetu huko Munich ni kufunga Bao na si kujihami!”
Nae Pep Guardiola amesema: “Ninaiamini kabisa Timu yangu, Tunaweza ikiwa tutacheza kitimu!”
Real wataingia kwenye Mechi hii bila ya Alvaro Arbeloa, Jese Rodriguez na Sami Khedira ambao wote wana matatizo ya Goti.
Bayern wao watawakosa Majeruhi Thiago Alcantara [ingawa amepona na Juzi kuanza Mazoezi], Holger Badstuber, Xherdan Shaqiri na Tom Starke.
Wachezaji ambao watacheza Nusu Fainali hii kwa wasiwasi wa wao kupata Kadi za Njano na hivyo kuikosa Fainali ikiwa Timu yao itafuzu ni Straika wa Bayern, Mario Mandzukic, na Wachezaji wa Real, Sergio Ramos, Xabi Alonso na Asier Illarramendi.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Bayern Munich (4-2-3-1):
Neuer;
Lahm, Dante, Boateng, Alaba;
Schweinsteiger, Kroos;
Muller; Ribery, Robben;
Mandzukic
Real Madrid (4-2-3-1):
Casillas;
Carvajal, Ramos, Pepe, Coentrao;
Alonso, Modric;
Di Maria, Ronaldo, Bale;
Benzema
REFA: Pedro Proença  (Portugal)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
Bayern Munich/Real Madrid v Chelsea/Atletico Madrid
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Powered by Blogger.