Ukraine; Warusi zaidi wawekewa vikwazo
Marekani imetoa taarifa kuhusu
vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi na kuushutumu utawala wa
Moscow kwa kushindwa kutimiza mkataba wa kimataifa uliolenga kusuluhisha
mzozo wa Ukraine.
Vikwazo hivyo vimelenga washirika wa Karibu wa
Rais wa Urusi Vladmir Putin na vimeongeza orodha ya vikwazo vilivyowekwa
hapo awali kwa baadhi ya maafisa wa nchi hiyo baada ya Moscow kutwaa
eneo la Crimea mwezi uliopita.Karibu asilimia sitini ya kampuni hiyo inamilikiwa na kampuni ya mafuta ya uingeza BP na thamani ya hisa za kampuni hiyo ilishuka punde tu baada ya taarifa kuhusu vikwazo hivyo kutolewa.
Wengine waliolengwa ni Alexei Pushkov, ambaye huongoza kamati ya mambo ya nje katika bunge la Urusi,Naibu waziri mkuu na kampuni kumi na saba za Urusi.
Akizungumza hapo awali Rais Putin alisisitiza kuwa Ukraine haitaathirika kiuchumi kutokana na vikwazo hivyo.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema nia ya Marekani sio kumlenga moja kwa Rais Putin lakini ni katika juhudi za kuishawishi Urusi kufuata mwelekeo unaofaa.
Muungano wa Ulaya pia umetangaza vikwazo vya usafiri na kuzuiliwa kwa mali dhidi ya watu 15 nchini Urusi lakini majina yao bado hayajatajwa.