Kuhusu milipuko minne iliyotokea Kenya Weekend iliyopita.
Mei 3 majira ya saa 2 usiku milipuko miwili yalitokea kwa mpigo Mjini Mombasa moja katika eneo la Nyali hoteli ya Reef iliyomuua mtu mmoja na nyingine eneo la kituo cha mabasi cha Mwembe tayari .
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kwamba mtu aliye kua katika gari aina ya Toyota Probox Alirusha bomu kuwalenga wasafiri walio kua wakisubiri kufika kwa basi.
Jumapili Mei 4 jiji la Nairobi watu 3 waliaga dunia na wengine 60 walijeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili kwenye mabasi mawaili tofauti katika barabara ya Thika super Highway jijini humo,mlipukohuo unasemekana ulitokana na vilipuzi vya IEDS vilivyokua vimewekwa katika mabasi hayo yaliyo kua yakiwasafirisha watu kutoka katikati mwa Jiji.
Hadi sasa wameripotiwa kufariki kwa watu 6 kufuatia shambulizi dhidi ya mabasi mawili jijini Nairobi na wanne Mombasa,baada ya shambulizi kwenye kituo cha mabasi mwembe tayari na katika hoteli ya Reef kule Nyali.
Kenya imekabiliwa na zaidi ya mashambulizi 80 na watu 300 wamefariki tangu wanajeshi wa Kenya kuanza kuwakabili wanamgambo wa Alshabaab kule Somalia.