Akichangia makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Augustine Mrema (MB,
Vunjo, TLP) amependekeza askari polisi wapewe asilimia 10 ya thamani ya
mali wanayokamata ili iwe kichocheo cha kufanya kazi kwa bidii na kuacha
kuomba na kupokea rushwa.