Mwenyekiti
wa baraza la vijana wa CHADEMA taifa(BAVICHA) John Heche,akiwa katika
mkutano wa hadhara wa UKAWA uwanja wa Shycom manispaa ya Shinyanga jana
jioni,ambapo alisema CCM ikianguka watu wengi wataumia kwa kuwa ni
mafisadi na kuwataka watanzania kuunga mkono UKAWA ili waweze kuing'oa
madarakani.
Alisema rasmu ya katiba
iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba inastahili kupongezwa kwa
kuwa ilifanya kazi kubwa ya kukusanya maoni ya watanzania na kuyafikisha
bila kuficha likiwemo suala la serikali tatu ambazo wanaziunga mkono. |