WABUNGE 25 WA CCM, CUF, CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI WAHAMA VYAMA VYAO NA KUJIUNGA NA CHAMA KIPYA CHA ACT
Mbali
na kuwanasa wabunge hao wa CHADEMA pia kimefanikiwa kuwavuta
wabunge wanne kutoka chama cha Mapinduzi ( CCM ),huku kikiwa na
uhakika wa kuwachomoa wabunge watatu kutoka NNCR-Mageuzi....
Tangu
kuanzishwa kwake mapema mwaka huu,ACT- Tanzania kimeonekana kuwa
chama cha upinzani cha kupambana na CHADEMA tofauti na vyama
vingine ambavyo dhamira zao ni kuing'oa CCM madarakani....
Chama
hicho kimekuwa kikiweka matawi yake kwenye maeneo
yanayotawaliwa na CHADEMA mkoani KIGOMA na kwenye baadhi ya
mikoa nchini...
Katibu
wa ACT kanda ya magharibi,Wiston Moga alinukuliwa akisema kuwa
lengo la chama hicho ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa
siasa, na wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo
la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambao ni chachu ya vyama
vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.....
Msemaji
wa CHADEMA,Tumain Makene aliwahi kunukuliwa akisema kuwa hatua
ya chama hicho kupingana na chama chao haina mantiki kwani
kinaonekana kukosa mwelekeo mapema...
"Tunajua
lengo lao ni lipi, wanachokifanya hakitawasaidia, ni vibaraka tu
hao, nia yao ni kuidhoofisha CHADEMA, jambo ambalo hawataliweza" Alisema Makene
Kwa
upande wake katibu mkuu wa ACT,Samson Mwigamba alisema
anaamini ipo orodha ndefu ya wanachama wa vyama mbalimbali vya
siasa ambao wako tayari kujiunga na chama chao ...