CHADEMA MKOA WA IRINGA YAZIDI KUPATA PIGO
Selemani Kiponda akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga |
Kisha akakabidhi bendara ya chama hicho iliyokuwa imetundikwa nyumbani kwake |
baadaye akatawazwa kwa kupewa kadi ya CCM na Diwani wa Kata ya Ihimbo,Hezron Nganyagwa (CCM) |
Na kisha akapewa bendera ya CCM ili akaipandishe nyumbani kwake |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) mkoani Iringa kinazidi kubomoka pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa
na viongozi wake katika kukiimarisha.
Naye diwani wa kata ya Ihimbo HezronNganyagwa aliahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali Kiponda ili kwa pamojawaweze kutekeleza vyema Ilani ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi wakata hiyo na Kilolo kwa ujumla.