Header Ads

HII HATARI!!!!!!! POMBE YA KIENYEJI YALETA MADHARA KWENYE FAMILIA YA WAPENDANAO

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi
Na Emanue lMadafa,Mbeya

Mwanamke mmoja Mkazi wa kijiji cha Mkutano Ndugu Mariana Simtowe  (32) anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kumuuwa mume wake Ndugu Petro Mteka (33) Mkazi wa kijiji cha mkutano kwa kumpiga kwa kipande cha mti.

Tukio hilo limetokea Julai 13mwaka huu  majira ya saa 21:00 usiku huko katika kijiji cha mkutano. Kata ya Nzoka,  wilayani  ya Momba, Mkoa wa Mbeya.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa akiwa njiani na marehemu mume wake wakitokea kilabu cha pombe za kienyeji wakiwa wamelewa ilitokea hali ya kutoelewana [ugomvi) na ndipo mtuhumiwa alipo tumia kipande cha mti na kumpiga nacho mume wake na kumsababishia majeraha.

Kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata mwanaume huyo, alipelekwa katika zahanati ya kijiji cha mkutano kwa matibabu na alifariki dunia mnamo tarehe 14.07.2014 majira ya saa 09:00 asubuhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Polisi Ahmed z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya unywaji wa pombe kupita kiasi kwani ni hatari kwa afya zao na huleta madhara katika jamii.

Aidha anatoa wito kwa wana ndoa kutatua migogoro yao kwa njia ya kukaa meza moja ya mazungumzo ili kupata muafaka.
MWISHO
Powered by Blogger.