SHEIKH ALIYELIPULIWA KWA BOMU ARUSHA ALITOA TAARIFA KABLA POLISI BAADA YA KUTISHIWA KUUAWA
Matukio
ya milipuko ya mabomu yameendelea kuuandama mkoa wa Arusha ambapo hapo
jana majira ya saa tano Usiku katika eneo la Majengo ya chini jijijni
Arusha kumetokea mlipuko wa bomu linalosadikiwa kuwa ni la kutengenezwa,
nyumbani kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Answar Suna Youth Center Shekh
Sudi Ali Sudi.