Katiba ya nchi haiwezi kuandikwa bila maridhiano ya makundi yote.
Sitakwenda Dodoma licha ya ushauri mbalimbali kwamba nikasemee ndani.
Nitakwenda kwenye Bunge la Katiba pale tu nitakaporidhika kuwa kuna
maridhiano baina ya makundi na wadau. Ushauri wangu ni kusitisha Bunge
Maalumu na kukubaliana maeneo kadhaa ya kurekebisha katika Katiba ya
sasa kisha tupate muda wenye utulivu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015
ili kuandika Katiba Bora. Umoja wa Katiba Bora yenye ridhaa ya wananchi
ndio kupona kwa nchi yetu dhidi ya machafuko. Wenye kudhani Katiba ni
sawa na ushabiki wa Simba na Yanga wasubiri Ligi Kuu ianze waende
Uwanjani kushabikia.
MANENO YA ZITTO KUHUSU MSIMAMO WAKE JUU YA BUNGE LA KATIBA
Reviewed by
Unknown
on
1:42 PM
Rating:
5