HII HATARI!!!!MTANDAO MWINGINE WA MAUAJI YA WANAWAKE WAIBUKA ARUSHA
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Lebaratusi Sabas amesema
tayari wameshaanza kukabiliana na wimbi hilo ambalo wauaji
wanapotekeleza azma yao hutokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu
chochote.
Kamanda Sabas ametaja mwanamke aliyeuwa kuwa ni Samimu Rashidi
aliyepigwa risasi na kufa papo hapo akiwa ndani ya gari lake tukio
lililotokea katika eneo la kwa Iddy jijini Arusha na mwingiene
aliyetajwa kwa jina la Flora Porokwa aliyepigwa risasi katika eneo hilo
hilo na kwa mazingira hayo hayo.
Aidha kamanda Sabas amesema hakuna mtu aliyekamatwa na wanaendelea
kuwatafuta watu wanaojihusisha na mtandao huo na amewaomba wananchi
kutoa ushirikiano.
Katika hatua nyingine idadi ya watuhumiwa wa mtandao wa milipuko
ya mabomu na kuwamwagia viongozi wa dini tindikali imeongezeka baada
ya watu watuhumiwa wengine wanne kukamatwa wakidaiwa kujihusisha na
mtandao huo.
Wakati huohuo watuhumiwa 16 wanaohusishwa na ulipuaji wa mabomu
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wamepandishwa kizimbani kwa
mara sita katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha.
Hadi sasa watuhumiwa zaidi ya 40 wanaohusishwa na mtandao wa
kulipua mabomu na kuwamwagia viongozi wa dini tindikali
wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani na bado msako wa kuwatafuta
wengine akiwemo anayedaiwa kuwa kinara wa mtandao huo Yahaya Hassan
Hela unaendelea.
NA ITV.CO.TZ