MAKUNDI YA UCHAGUZI MKUU UJAO YAITESA CCM MKOANI KATAVI WASIMAMISHA VIONGOZI WAO
Hari ya siasa ndani ya uongozi wa CCM Mkoani Katavi si shwari kutokana na mgawanyiko wa makundi yaliopo ya watu watakao kuwa wanagombea nafasi ya ubunge kupitia
chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 hari ambayo imepelekea
baadhi ya viongozi kusimamishwa yadhifa zao na wengine kupewa onyo
Makundi
hayo yamedhihililika hivi karibuni katika kikao cha kamati ya siasa cha
Mkoa wa Katavi kilichofanyika hivi karibuni na kutowa uamuzi wa
kuwasimamisha baadhi ya viongozi wake ambapo ndani yakikao hicho baadhi ya wajumbe walitaka viongozi hao wasisimamishwe
Viongozi waliosimamishwa ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Mpanda Joseph Lwamba ambae anatuhumiwa kuwa amekuwa akikwamisha shughuli za Chama na kukisema chama hicho vibaya
Pia katika barua zao walizokabidhiwa juzu zilizoandikwa septemba 1 mwaka huu katibu mwenezi huyo anatuhumiwa kushindwa kuwahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye mapokezi na mikutano ya
hadhara wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Abdalamani Kinana wakati wa
ziara yake wilayani Mpanda mwaka huu na kusababisha wajitokeze wananchi
wachache
Kiongozi mwingine aliyesimamishwa ni mjumbe wa kamati ya siasa wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mpanda Beda Katani
Yeye amesimamishwa ujumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa kwa kile anachodaiwa kuendesha kampeni za mtu mmoja ambae anania ya kugombea ubunge wa jimbo la Mpanda Mjini kupitia CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao
Pia Kamati ya Siasa hiyo ya Mkoa imemwandikia barua za onyo Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Katavi (CCM) Dr Pudensiana Kikwembe kwa kutoridhika kwao na mwenendo wake kwenye jamii
Kwa
mujibu wa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alimweleza mwandishi wa
habari hizo kuwa kikao hicho kimemwandikia barua ya onyo Galus Mgawe
ambae anatuhumiwa kuanza kampeni za kugombea ubunge wa Jimbo la Mpanda
Mjini kabla ya muda wake kuwa umefikia
Kumekuwepo na mgawanyiko ndani ya Chama hicho kwenye wajumbe wa kamati ya siasa za Wilaya ya Mpanda na kamati ya Siasa ya Mkoa ambapo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakishutumiana kuwa kuna wagombea ambao pande hizo mbili zinawafanyia kampeni za ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ninaloongozwa na Mbunge wa sasa Said Arfi (CHADEMA)aliyeliongoza kwa vipindi viwili sasa
Makundi hayo yalijidhihirilisha wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Abdalamani Kinana ambapo baadhi ya viongozi walitupiana maneno ya kushutumiana mbele ya Kinana na baada ya kushutumiana Mwenyekiti wa CCM wa wIlaya ya Mpanda na Katibu mwenezi wake waliacha kwenda ofisini kwa kile walichokuwa wakidai katibu wa chama wa Wilaya Hamida Mbogo apangiwe kituo kingine cha kazi kwani yeye amekuwa akirudisha nyuma shughuli za chama
Mmoja wa viongozi ho waliosimamishwa Joseph Lwamba amekiri kupokea barua ya kusimamishwa kwake ingawa barua hiyo amedai inamakosa kwani inaonyesha barua hiyo imeandikwa Sptemba 1 mwaka 2001 bada ya septemba 1 mwaka huu