Header Ads

HUYU NDIYE KIJANA ANAYETIKISA AFRIKA MASHARIKI KATIKA TASNIA YA NYIMBO ZA INJILI.


 Tasnia ya Nyimbo za Injili Tanzania Inaweza kukumbwa na Mageuzi makubwa kutokana na Baadhi ya Wasanii wa Music huo hasa wa Kizazi kipya kuonekana kuja kwa njia tofauti na kuwavutia wasanii mbalimbali nchini na Afrika Mashariki.


Mmoja wa Wasanii hao ni pamoja na Eng CARLOS MKUNDI kutoka Jijini  Arusha ambaye ambaye anatamba na vibao vyake vingi ikiwemo wimbo wake wa nimetoka mbali ambao unaonekana kuwagusa mashabiki wengi wa nyimbo za Injili Afrika Mashariki.

Mwanamziki huyo anaonekana kuja kasi hasa kwakuandaa matamasha makubwa ya dini na kuwa shirikisha Wasanii wakubwa Hapa nchini jambo ambalo linakuwa ni vigumu kwa wasanii wengine.

Katika kuwaonyesha wapenzi na Mashabiki wake kuwa anawajali lakini pia anatambua mchango wa familia yenye amani na mafanuikio ameandaa Tamasha kubwa lijulikanalo kama UPENDO KWA MAMA ambalo liafanyika  Mkoani Arusha kuwasaidia wakina MAMA wanoishi katika mazingira magumu.

Tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Shekn Amri Abed Karume Mkoani Arusha nahudhuriwa na umati mkubwa wawatu tofauti na matamasha menginge waliyowahi kufanyika hapa nchini Tanzania na kuwashirikisha wasanii kutoka Afrika Mashariki na Kati.
Powered by Blogger.