TUAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI MAMA ALIYEUA MTOTO WAKE KWA KUMCHINJA NAYE ACHINJWA NA WANANCHI HUKO MARA
![]() |
Mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa kwa mapanga na wananchi wenye hasira kali kwa kitendo alichokifanya cha kumuua mtoto wake wa kambo kwa kumchinja kwa panga. |
![]() |
Mwili wa mtoto aliefariki kwa kuchinjwa na mama ake wa kambo kwa kutumia panga linaloonekana hapo chini pichani. |
Tukio
lilitokea hivi karibuni mkoani Mara la mama wa kambo kumchinja mtoto
wake kwa kutumia panga hadi kufariki, limechukua sura mpya baada ya mama
huyo nae kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kukatwa katwa
na mapanga mpaka kufariki.
Tukio
la kukatwa katwa mapanga mama huyo limetokea baada ya wananchi wa
kijijini hapo walioshikwa na jazba kali kwa kutokubaliana na kitendo cha
kinyama alichomfanyia mtoto huyo kwa kumkatishia maisha yake.
Hata
hivyo wananchi walionekana kujichukulia hatua mikononi kwa kumuua mama
huyo, kwa kile kilichodaiwa hawakuona hatua zozote za kisheria
alizochukuliwa mtuhumuwa huyo kwa kitendo cha kinyama alichokifanya.
Awali
mwenyekiti wa kijiji alifatwa na wanakijiji kuulizwa ni hatua gani ya
kisheria mtuhumiwa atachukuliwa kwa mauaji ya kinyama aliyoyafanya
kwamaana baada ya tukio, mtuhumiwa alionekana kutochukuliwa hatua yeyote
ya kisheria kwa muda mrefu licha ya serikali ya kijiji na polisi kupata
taarifa ya kutokea tukio hilo.
Mwenyekiti
wa kijiji aliwajibu wanakijiji kuwa polisi wanatambua kutokea kwa tukio
hilo na watakuja kumkamata mtuhumiwa na hatua za kisheria za mauaju
zote zitafata juu yake.
Muda
ulizidi kutokomea bila kuonekana dalili zozote za mtuhumiwa huyo
kuchuliwa hatua, ndio wanakijiji wenye hasira kali walipomvamia mama
huyo na kumkatakata kwa mapanga kulipiza kisasi kwa kile alichomfanyia
mtoto wake.