MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA ARUSHA AWATAKA WANAKWAYA KUWA WABUNIFU ZAIDI ILI KUJIAJIRI WENYEWE.
picha na matukio mbalimbali yaliyojiri jana juma pili katika uzinduzi wa kwaya ya Yerusalemu ya kanisa la Tanzania Assebly of God lililopo Lemara jijini Arusha
Wananchi nwa mkoa wa Arusha wameshauriwa kujiajiri na kujiunga na vikundi vidogovidogo vya ujasiria maili ili kuepuka ukiukwaji wa maadili pamoja na kufanya vitendo viovu hasa kwa vijana ambao ni taifa ya leo na kesho.
Hayo yamesemwa na mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Bw Gaudens Lymo wakati akizindua kwaya ya Yerusalem ya Kaniasa la TAG lemara ambapo amehimiza swala zima la kujishughulisha katika shughuli mbalimbali pamoja na kumtumikia Mungu kiroho.
Bw,Lymo amesema kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa serikali inathamimini vikundi vya ujasiria mali kwakuwa vimekuwa mkombozi kwa jamii nyingi hapa nchi na hivyo kuwapatia asilimia 10%ya mapato yanayokusanywa na Halmashauri ili kuvikuza na kuviendeleza vikundi hivyo hapa nchini.
Amesema kutokana na kujishughulisha huko kutasaidia jamii kuweza kusomesha Watoto,kuwa na Afya nzuri vilevile kiuchumi.
Pamoja na hayo pia amelitaka kanisa hilo kuwa wabunifu ili kuweza kuwa na vitega uchumi mbalimbali ambavyo vitakuwa na msaada mbalimbali kwao na kwa jamii kiujumla.
Sambamba na hayo amewapongeza wanakwaya wa Yerusalemu kwa kazi kubwa waliyoifanya hasa katika uimbaji kwakuwa inawajenga watu kiroho na kimwili kwani wakati mwingi hutoa faraja.
Kwa Upande wa Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Mch,Wilsoni Lyakunda amewataka wana kwaya hao kutokukata tamaa licha ya changamoto wanazokutana nazo na kutambua kuwa kazi ya Mungu siku zote inamalipo yake.
Pia amewashukuru waumini pamoja na wanakwaya kutoka makanisa mbalimbali kwa kuweza kushirikiana nao bega kwa bega na kuhakikisha wanafanikiwa katika uzinduzi huo wa awali ambapo ni Albamu yao ya kwanza ambayo inajumla ya nyimbo tisa inayojulikana kwa jina la MUNGU MUUMBA WA VYOTE.