Header Ads

Eng;Carlos Rais wa kina mama awa gumzo,ateka hisia za waumini na wapenzi wa njimbo za injili Arusha.













 

 Baadhi ya waumini wa kanisa la TAG Lemara wakifurahi kwa pamoja wakati Eng Carlos Mkundi anaimba wimbo wa nimetoka mbali.

Picha za matukio mbalimbali

Msanii wa nyimbo za injili nchini Tanzania anayekuja kawa kasi Eng;Carlos Mkundi ameonekana kuteka hisia wa watu mbalimbali pamoja na wapenzi wa nyimbo za injili Tanzania na nje kwakuweza kushangiliwa na umati mkubwa mara baada ya kuhudhuria Uzinduzi wa Kwaya ya Yerusalemu ya kanisa laT.A.G Lemara Arusha.



Tukio hilo la umati wa waumini waliohudhuria katika uzinduzi huo ulitokea jana jumapili ambapo Eng; Carlos Mkundi alikuwa ni moja kati ya watu waliohudhuria Uzinduzi huo ambapo mgeni Rasmi alikiwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Bw Gaudensi Lymo.

Carlos ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Raisi wa upendo kwa mama kutokana na kuanzisha mfuko unaojulikana kama UPENDO KWA MAMA FOUNDATION pamoja na kuandaa matamasha mbalimbali ya nyimbo za Injili pia liitwalo Upendo kwa mama Amekuwa kuvutio cha watu wengi kutokana na kuwajali na kuwapenda wakina mama wao ishi katika mazingira magumu kwakuwasaidia kichumi nk.

Kila mtu aliyekuwepo katika tamasha hilo walimtaka aweze kuimba ambapo aliweza kuzikonga nyoyo wa waumini hao alipoimba wimbo wa nimetoka Mbali.,

Aidha Bw Carlos alipo hojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na wito wake wa kuanzisha upendo kwa mama alidai kuwa wakina mama ndio watu muhimu katika jamii vilevile ndio wenye majukumu makubwa ya kuhakikisha watoto wanapata Afya njema,Elimu pamoja na Malazi na kusema kuwa atapigana hadi hatua ya mwisha mpaka wakina mama waweza kuthaminiwa katika jamii.

Kwa upande wa Stahiki meya wa Jiji la Arusha Bw,Gaudens Lymo amempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaka kutokukata tamaa na kuahidi kushirikiana nae bega kwa bega
Powered by Blogger.