WAZIRI PINDA : TUTAUNGANISHA NGUVU KWA MGOMBEA URAIS ATAKAYE TEULIWA NA CHAMA
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi wa tarafa ya pawaga leo |
Wananchi wa tarafa ya pawaga Iringa wakimsikiiza waziri mkuu Bw Pinda |
Wananchi wa tarafa ya Pawaga wakimshangilia waziri mkuu Pinda leo |
Waziri mkuu akiwapungia mikono wananchi wa tarafa ya Pawaga leo |
Pinda Waziri Pinda alitoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa tarafa ya Pawaga Baada ya kuzindua skimu ya umwagiliji itakayowanufaisha wakazi wa vijiji vitatu kikiwemo cha Magozi,Ilolompya na Mkombilenga uliogharimu zaidi ya Tsh bilioni 1.6 fedha kutoka kwa wahisani na serikali.
Alisema kuwa utaratibu wa ndani ya chama anbacho wao ni watawala na wanaoendelea kuyafanya maendeleo yanaonekana watalazimika kumuunga mkono atakayeteuliwa na wale wote ambao hawajateuliwa watamuunga mkono atakayeteuliwa kwa makundi yote kuvunjwa na kuwa na Kundi moja pekee.
Kuwa wapo wapotoshaji ambao watafika na kuwadanganya juu ya katiba hiyo inayopendekezwa na wasiwasikilize
Katika hatua nyingine Waziri mkuu Pinda amewataka wakulima wa mpunga Pawaga katika kuepuka na migogoro kati yao na wafugaji kuweka utaratibu wa kukusanya majani ya mpunga na kuyapeleka majumbani kwao ili wafugaji wapate kununua kuliko kuyaacha mashambani na kuwafanya wafugaji kuingiza mifugo Yao mashambani.