MISWADA MIWILI YA HABARI YA MWAKA 2015 YAONDOLEWA BUNGENI
Juhudi za wadau wa habari kuwasilisha
ombi kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda wakitaka miswada miwili ya habari ya
mwaka 2015 iwasilishwe kwa mfumo wa kawaida, zimezaa matunda baada ya Serikali
kuamua kuiondoa kabisa miswada hiyo, sasa haitajadiliwa tena katika mkutano wa
19 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
“Hilo linaweza kufanyika hapahapa Dodomamaana miswada hii inajadiliwa wiki ijayo na kupitishwa. Hilo lisipofanyikakutakuwa na malalamiko makubwa na huenda tukapitisha sheria ambayo baadayetutalazimika kuiboresha.”