Radi yaua watu wanane na wanafunzi 6 wa shule ya msingi kibirizi na kujeruhi 15 manispaa ya Kigoma.
WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi kibirizi
Manispaa ya Kigoma wamekufa baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa kigoma
Maweni,DK.FADHILI KIBAYA amesema sambamba na watu hao waliofariki pia
watu 15 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Dk.Kibaya amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Yusuf Athuman,
Hassan Ally, Fatuma Sley, Zamda Seif, Shukrani Yohana na Warupe Kapupa
ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule hiyo ambapo Mwalim
aliyefariki ametambuliwa kwa jina la Elieza Mbwambo aliyekuwa
akifundisha darasa la tano.
Aidha pamoja na watu hao mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina la
Focas Ntahamba pia amefariki kwa kupigwa na radi katika eneo la Bangwe
mjini kigoma.
Mmoja wa walimu wa shule ya msingi ya kibirizi,WILBERT EMANUEL
ambaye alikuwepo eneo la tukio amesema kuwa wamesikitishwa na tukio hilo
ambalo lilitokea bila kutegemea na kuacha simanzi kubwa shuleni hapo.
Hili ni tukio la pili kutokea mkoani kigoma ambapo takriban mwezi
mmoja uliopita wanafunzi sita na mwalim wao walikufa baada ya
kupigwa na radi katika shule ya msingi nyakasanda katika kijiji cha
nyachenda wilayani kasulu.