RUSHWA YA NGONO NI UNAJISI:
Waajiri wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuendekeza
vitendo vya ngono kwa lengo la kuwapa ajira mabinti ambao wanalazimiswa kutoa
rushwa ya ngono kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kujitia unajisi mkubwa.
Hayo yamesemwa na Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili
Eng:Carlos Mkundi wakati akitoa maoni yake katika sikuku ya wafanyakazi
duniani ambapo amesema kumekuwa na watu wenye nyadhifa katika makampuni na
Mashirika mbalimbali ambao wanatumia fursa hiyo kuomba rushwa ya Ngono.
Amesema kuwa kufanya kitendo hicho kunasababisha mbegu ya
unajisi kuzaliwa katika eneo hilo na hata pindi binti ama mtu huyo kupata kazi
kunakuwa hakuna faida ndania ya Kampuni yao kutokana na kuwepo na roho ya
Unajisi ndani yao.
Aidha Eng:Carlos amesema ni vyema nafasi za kazi zikatolewa
kwa utaratibu na heshima au kama zinavyo elekeza sheria za nchi na wala siyo
vinginevyo na kudai kuwa kunapokuwa na halikama hiyo taarifa zitolewe katika
eneo husika ili atua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Pamoja na hayo amewataka mabinti pamoja na wakina Mama
kutokukata tama katika kutafuta fursa mbalimbali zakiuchumi ili waweze kujikimu
katika mahitaji yao.
Sambamba na hayo Amesema ni vyema mabinti kuacha
kujirahishisha kwa kutoa miili yao kutokana na kutokuwa na ajira na badala yake
wanapaswa kuwa na tumaini na subira huku wakimuomba Mungu.