Header Ads

WIMBO WA INJILI WA "MUNGU AMESEMA NDIO" KUZINDULIWA MWISHONI MWA MWEZI JANUARI MWAKA.


















 












WIMBO mpya wa Injili wa MUNGU AMESEMA NDIO kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu wimbo wa  MUNGU AMESEMA NDIO umeimbwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili ajulikanae kama Mhandisi Carlos Mkundi (Pichani).


Hayo yamesemwa na mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili wakati akizungumza na mwandishi wa MICHUZI BLOG jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa baada ya kutoa wimbo wake wa MUNGU AMESEMA NDIO atatoa wimbo wa mwingine ambao ameupa jina la YOU ARE THE SAME YOU NEVER CHENGE ambao ataimba kwa lugha ya kiingereza ili watu mbalimbali waweze kuusikia.

Mhandisi Mkundi ameimba nyimbo za Injili mbalimbali zinazojulikana kama Nimetoka mbali, Wewe ni Mungu, Usinishike bega, Moyo wangu wakuabudu.
Aidha amewaomba wananchi na wadau wa nyimbo za Injili hapa nchini wamuunge mkono ili kutangaza neno la Mungu kwa mataifa yote kupitia nyimbo za Injili.

Powered by Blogger.