Haya hapa mambo sita aliyoyaongea Mo Dewji kuhusu simba
Jina la mkurugenzi mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) ambaye pia ni bilionea kijana Afrika Mohammed Dewji ‘MO’linazidi kuiingia kwenye headlines kila kukicha kutokana na biashara zake na kutoa ajira kwa watu zaidi ya 20,000, leo July 29 MO amezungumzia mpango wake kuinunua Simba.
Mohammed Dewji ameweka wazi mambo 6 kuhusiana na mpango wake wa kutaka kununua hisa asilimia 51 za Simba na faida watakayopata wanachama wa Simba baada ya Mohammed Dewji kuinunua klabu hiyo. Naomba nikusogezee mambo 6 aliyoyaongeaMohammed Dewji katika mpango wake wa kutaka kuinunua Simba.
1- Sababu za Simba kutofanya vizuri ni kutokana na bajeti, mfano Yanga bajeti yao inaweza kufikia bilioni 2.5 sawa labda na Azam FC wakati bajeti ya Simba inaweza kuwa nusu ya bajeti za washindani wake.
2- Simba kwa sasa haihitaji mdhamini ili kuweza kujiendesha au kutegemea kwa maana mpira unahitaji pesa sio mdhamini atakayetoa milioni 400 au chini ya hapo.
3- Wanachama wa Simba wa muda mrefu watapewa hisa bure na sio kujivunia kadi ya uanachama isiyoingiza kitu chochote, utakuwa na uwezo wa kuuza hisa zako au kununua nyingine kama utahitaji.
4- Simba kwa sasa inatakiwa iwe mbali ya hapo ilipo kwani sasa inatimiza miaka 80 toka ianzishwe kwake mwaka 1936, lakini haina hata uwanja wa mazoezi tumezidiwa hata na Azam FC wameanza juzi.
5- Nilijitoa African Lyon ni baada ya kwenda uwanjani na kuona timu haina mashabiki mpira unahitaji mashabiki, hata Simba kama isingekuwa na mashabiki nisingeingia mpira unahitaji mashabiki, kuhusu Singida United niliidhamini ikaingia Ligi Kuu zikaanza siasa nikaamua kujitoa.
6- Mimi dhamira yangu sio kupata pesa kutoka Simba nashukuru mungu amenijalia sana nina biashara zaidi 100 tumeajiri watu 28000 na tutaendelea kuajiri zaidi, dhamira yangu kuona Simba inasonga mbele zaidi.