Header Ads

Licha ya kuwa mahiri uwanjani, darasani walikuwa vizuri, hawa ni mastaa wa soka wanne wenye degree

Huenda unawafahamu nyota kadhaa wa soka duniani na baadhi ya vitu vyao vya thamani wanavyomiliki kutokana na vyombo vingi vya habari hupenda kuviandika na vingine huwa havizungumzwi kabisa, najua ushawahi kusikia rekodi za mastaa wengi wa soka ambao walikuwa wanafanya vizuri uwanjani, darasani walikuwa hawafanyi vizuri.

Lakini leo November 30 naomba nikusogezee list ya mastaa wanne wa soka ambao wana elimu ya kuanzia ngazi ya degree, hawa sio tu ndio waliokuwa na elimu pekee huenda wakawepo wengine ila list hii ndio millardayo.com imefanikiwa kuipata na naomba nikusogezee mtu wangu wa nguvu.
1- Frank Lampard huyu ni staa wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza na Man City anatajwa kuwa katika list ya wachezaji soka wenye uwezo mkubwa uwanjani lakini pia alikuwa akifanya vizuri, kuna wakati wachezaji wenzake wa Chelsea walikuwa wanamuita Professor, anatajwa kuwa na elimu ya 11 GSCE.
147018
Frank Lampard
2- Edwin van der Sar alikuwa golikipa mahiri wa klabu ya Manchester United yaUingereza ila mwaka 2011 aliamua kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa 41. Edwin van der Sar ana elimu ya masters ya Marketing.
_49408413_vandersar
Edwin van der Sar
3- Joseph Owino huyu ni beki wa kati wa kimataifa wa Uganda na amewahi kuichezea klabu ya Simba kwa nyakati mbili tofauti, Owino ni miongoni mwa mastaa wa soka wenye elimu, yeye ana elimu ya masters ya Business Administration ya chuo kikuu cha Makerere.
kiungo
Joseph Owino
4- Michael Olunga kuna wakati aliwahi kuhusishwa na klabu ya Simba kutaka kumsajili staa huyo wa klabu ya Gor Mahia ya KenyaOlunga kwa sasa amekuwa akiingia katika headlines kutokana na kufunga magoli katika michuano ya Kombe la Challengeinayoendelea Ethiopia. Ukisikia mtangazaji anamuita engineer usishangae ni engineer kweli mwenye elimu ya degree kutoka Technical University of Kenya.
1698942hp2
Michael Olunga
Powered by Blogger.