Header Ads

Rais Magufuli afanya uteuzi wa makatibu tawala Rukwa na Mara

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Maguful
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.
Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.
Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.
Powered by Blogger.