Header Ads

VINCENT BOSSOU AREJEA KIKOSINI YANGA

BEKI tegemeo wa Yanga, Mtogo Vincent Bossou leo anatarajiwa kuanza mazoezi baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC.

Yanga ililazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC Jumatano Uwanja wa Nangwanda, Sijaona, Mtwara, siku ambayo Bossou mwenye asili ya Ivory Coast hakuwepo baada ya kuchelewa kurejea kufuatia ruhusa ya kwenda timu yake ya taifam, Togo. 

Bosoou aliyeiwezesha Togo kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Djibouti akiifunga bao moja The Sparrow Hawks, huku mengine yakifungwa na Mathieu Dossevi, Fo-Doh Laba na Komlan Agbegniadan mawili.

Togo imemaliza nafasi ya pili kwenye Kundi A hivyo kufuzu Afcon ya kwanza tangu mwaka 2013, baada ya Tunisia iliyoifunga Liberia 4-1 na kumaliza kileleni.

Wachezaji wengine waliokosekana kwenye kikosi cha Mholanzi, Hans van der Pluijm kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ aliyekuwa kwenye msiba wa baba yake, beki Pato Ngonyani waliokuwa majeruhi sawa na viungo Geofrey Mwashuiya na Haruna Niyonzima na mshambuliaji Malimi Busungu nao wanatarajiwa kurejea.

Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani kesho Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Maji Maji ya Songea katika mfululizo wa Ligi Kuu.

Na kikosi kizima cha Yanga leo kimefanya mazoesi ya asubuhi Uwanja wa Uhuru, Dar e Salaa ambako wanatarajiwa kurdui na joni ya leo.


Powered by Blogger.