Viongozi CHADEMA waazimia kutompa ushirikiano mkuu wa wilaya ya Njombe.
Viongozi wa chama cha Demokarasia na Maendeleo wilaya ya Njombe wametoa maazio ya kuto fanya kazi na mkuu wa wilaya ya Njombe ,Bi RUTH MSAFIRI kwa kile walichodai kuwa alimdhalilisha mwenyekiti wa mtaa wa Buguruni kwa kumchapa makofi February 28 mwaka huu akiwa ofisini kwake.
Uongozi wa chama hicho wilaya umekuja na tamko la pamoja na kumtaka mkuu
wa wilaya a N jombe kuomba radhi ndani ya siku 7 na la sivyo hatapewa
ushirikiano na vingozi wote wa chama hicho wakiwemo Wenyeviti wa Mitaa na
Madiwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa wenyeviti wa chama cha
CHADEMA, Bw.BARASION MGAYA amemtaka kiongozi huyo kuheshimu uongozi uliowekwa
na wananchi.
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi, RUTH MSAFIRI amekana kumpigia
mwenyekiti huyo na kusisitiza aliamuru vyombo vya ulinzi kumuweka ndani kwa
masaa 48 kwa kile alichodai kuwa ali toa lugha ya matusi dhidi yake.