BPL: MABINGWA MAN UNITED WABANWA, ARSENAL, CHELSEA HAOO..!
LIGI KUU ENGLAND
Saturday, 19 October 2013 19:37
>>MOURINHO APIGWA KADI NYEKUNDU!!
ARSENAL wameendelea kubaki kileleni mwa
BPL, Ligi Kuu England, baada ya kuichapa Norwich City Bao 4-1 Uwanjani
Emirates na Chelsea, waliokuwepo kwao Stamford Bridge, pia kuipiga Bao
4-1 Cardiff City na kukamata Nafasi ya Pili huku Mabingwa Manchester
United wakibanwa kwa Sare ya Bao 1-1 na Southampton ambayo imewaacha
wakiwa Nafasi ya 8.
PATA ZAIDI:
++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi 19 Oktoba
Newcastle United 2 Liverpool 2
[Saa za Bongo]
Arsenal 4 Norwich City 1
Chelsea 4 Cardiff City 1
Everton 2 Hull City 1
Manchester United 1 Southampton 1
Stoke City 0 West Bromwich Albion 0
Swansea City 4 Sunderland 0
[Saa za Bongo]
19:30 West Ham United v Manchester City
++++++++++++++++
EVERTON 2 HULL CITY 1
Bao za Kevin Mirallas na Steven Pienaar
zimewapa Everton ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Hull City ambao walifunga
Bao lao kupitia Yannick Sagbo.
VIKOSI:
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Barkley, Osman, Lukaku
Akiba: Robles, Jelavic, Kone, Deulofeu, Naismith, Pienaar, Stones.
Hull: McGregor, Rosenior, Davies, Faye, Figueroa, Elmohamady, Huddlestone, Livermore, Brady, Aluko, Graham
Akiba: Bruce, Meyler, McShane, Boyd, Sagbo, Harper, Quinn.
ARSENAL 4 NORWICH CITY 1
Bao za Jack Wilshere, Mersut Ozil, Bao 2, na Aaron Ramsey, zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 4-1 na kujikita kileleni mwa Ligi.
Bao pekee la Norwich City lilifungwa na Jonny Howson.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Koscielny, Mertesacker, Gibbs, Wilshere, Arteta, Flamini, Cazorla, Ozil, Giroud
Norwich: Ruddy; Martin, Bassong, Turner, Olsson; Tettey, Fer, Howson; Snodgrass, Pilkington, Hooper.
MAN UNITED 1 SOUTHAMPTON 1
Robin van Persie aliwapa Mabingwa Man
United Bao la kuongoza lakini katika Dakika ya 89 kona ilishindwa
kuokolewa na Phil Jones na Southampton kusawazisha kupitia Lovren.
Katika Mechi hii mara mbili Man United walipiga posti kupitia Wayne Rooney na Van Persie.
VIKOSI:
Man United: De Gea; Rafael, Jones, Evans, Evra, Nani, Carrick, Fellaini, Januzaj, Rooney, van Persie.
Southampton: Boruc, Clyne, Fonte, Lovren, Shaw, Wanyama, Schneiderlin, S. Davis, Lallana, Rodriguez, Osvaldo
CHELSEA 4 CARDIFF 1
Jordon Mutch alitangulia kuipa Bao
Cardiff City lakini Chelsea walijibu mapigo kwa kupiga Bao 4 kupitia
Hazard, Bao 2, Samuel Eto’o na Oscar ambazo ziliwapa Timu ya Jose
Mourinho ushindi wa Bao 4-1 na kuchupa hadi Nafasi ya Pili.
Hata hivyo Mechi hiyo iliingia utata
kwenye Bao la kusawazisha la Chelsea ambalo Kipa Marshall alidunda Mpira
chini baada ya kuudaka na Eto’o kuudokoa na baadae kumfikia Hazard
aliefunga lakini Wachambuzi wamebainisha kuwa Kisheria Goli hilo
lingetakiwa kutokubaliwa.
Mourinho alimaliza Mechi hii akiwa Mtazamaji baada ya kutolewa nje na Refa.
VIKOSI:
Chelsea: Cech; Ivanovic, D Luiz, Terry, Bertrand; Ramires, Lampard; Willian, Mata, Hazard; Eto'o
Cardiff: Marshall; Taylor, Caulker, Turner, Whittingham, Medel, Odemwingie, Gunnarsson, Mutch, Cowie, Theophile-Catherine.
SWANSEA 4 SUNDERLAND 0
Katika Mechi ya kwanza ya Meneja mpya
Gus Poyet wa Sunderland alieshika wadhifa baada ya kutimuliwa Paolo Di
Canio, Sunderland imebamizwa Bao 4-0 na Swansea ambao walipata Bao lao
la kwanza baada ya Phil Bardsley kujifunga mwenyewe.
Bao nyingine za Swansea zilifungwa na Jonathan De Guzman, Wilfried Bony, kwa Penati, na Chico Flores.
VIKOSI:
Swansea: Vorm, Rangel, Chico, Amat, Davies, Britton, de Guzman, Michu, Dyer, Routledge, Bony
Sunderland: Westwood, Celustka, Bardsley, O'Shea, Roberge, Cattermole, Johnson, Larsson, Gardner, Giaccherini, Fletcher.
STOKE CITY 0 WEST BROM 0
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Wilkinson, Shawcross, Huth, Pieters, Ireland, Nzonzi, Adam, Walters, Arnautovic, Assaidi
Akiba: Whelan, Palacios, Jones, Wilson, Crouch, Etherington, Sorensen.
West Brom: Myhill, Billy Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Yacob, Mulumbu, Amalfitano, Sessegnon, Berahino, Anichebe
Akiba: Morrison, Long, Brunt, Luke Daniels, Vydra, Dawson, Anelka.
RATIBA:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
[Saa za Bongo]
Jumapili 20 Oktoba
18:00 Aston Villa v Tottenham Hotspur
Jumatatu 21 Oktoba
22:00 Crystal Palace v Fulham