MEYA SILAA AJA NA KAMPENI KABAMBE YA KUCHANGIA MADAWATI KUPITIA SANAA
Saturday, October 19, 2013
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa (wa pili kushoto) akizungumza
na waandishi wa habari leo asubuhi kuhusu kampeni ya ‘Dawati ni Elimu’
kupitia wasanii mbalimbali wa kuchora nchini. Kulia kwake ni Msanii
Robin Mtila na Kushoto ni Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro,
Trevor Saldanha na Mustafa Hassanali Mratibu wa Kampeni hiyo.
Meneja
Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha akizungumzia mchango
wa hoteli yake katika kampeni ya Dawati ni Elimu yenye kauli mbiu ya
"Kalisha mmoja boresha Elimu".
Mchoraji
Robin Mtila akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake ambapo ameelezea
umuhimu wa sekta ya Elimu katika fani ya sanaa nchini.
Mkurugenzi
wa Advert Construction Ltd Dhmy Jog akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kampuni yake kuchangia Tsh 10 milioni kwenye kampeni hiyo ya
kuondoa tatizo la madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.
Baadhi wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha kubwa la Sanaa lenye lengo la kuchangia kampeni ya Dawati ni Elimu.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na
wasanii wa Sanaa ya Uchoraji pamoja na baadhi ya wadhamini wa kampeni
hiyo. .Kampeni ya Dawati ni Elimu yakusanya Tsh 1bilioni mpaka sasa lengo ni kufikia Tsh 4.98bilioni .atoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha la mwaka dawati ni elimu
Na Moblog Team
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa akishirikiana na Hyatt
Regency Kilimanjaro Hotel na wasanii kumi maarufu nchini wameandaa
tamasha kubwa la sanaa la mwaka kwa wasanii wa kuchora (Painters) lenye
lengo la kuchangia kampeni ya “Dawati ni Elimu” katika shule za msingi
na sekondari jijini Dar es Salaam.
Moblog linaripoti Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mhe Silaa amesema kuwa
katika kampeni hiyo ya ‘Dawati ni Elimu’ kupitia programu ya (Annual
Mayors Charity Ball) wameamua tarehe 16 ya mwezi Novemba kuwa na tamasha
la sanaa ya uchoraji itakayowashirikisha wasanii kumi maarufu nchini.
“kwenye
tamasha la tarehe 16 mwezi Novemba mwaka huu wasanii wa kuchora
wataweza kuchora picha mbalimbali kwa ubunifu wao na kuweza kuonyesha
kazi zao pamoja na kuuza kwa wateja katika Hoteli ya Hyatt Regency
Kilimanjaro Hotel na sehemu ya mapato yatachangia madawati na asilimia
zingine itakuwa faida yao baada ya mauzo kwenye maonyesho ya picha ,”
amesema.
Amesema
kuwa katika tamasha hilo la sanaa ya kuchora wasanii wataweza kuonyesha
kazi zao za sanaa katika harakati za kuhamasisha jamii kuchangia
kupunguza tatizo la madawati kwenye shule za msingi na sekondari kupitia
kauli mbiu ya “Kalisha mmoja, boresha elimu”
Silaa
aliongeza pia kwamba katika tamasha hilo la mwaka pia kutakuwa na
chakula cha mchana kwa wageni wote wataohudhuria Shughuli hiyo ambayo
itakuwa ya wiki nzima katika kuhakikisha lengo hilo la kupata madawati
kwenye shule linafanikiwa. Amesema
kuwa kwa sasa takwimu zinaonyesha asilimia 30 ya wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari wanakaa chini kwa kukosa madawati katika shule
nyingi za kata mkoa wa Dar es Salaam.
Alisisitiza
kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya
Ilala wanatafuta njia bora ambayo wachangiaji wanaweza kuchangia kupitia
mitandao ya simu ili kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa hiyo
adhimu na pesa za wananchi zinafanya kazi iliyokusudiwa.
“watanzania
ni lazima waamke ili waweze kuchangia maendeleo ya elimu nchini katika
kusukuma mbele maslahi mapana ya nchi kwa siku za usoni ili taifa letu
liweze kuwa na wananchi waliopata elimu bora na si bora elimu,”
alisisitiza Mhe Silaa .Kwa upande wake Meneja
Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha amesema kuwa ni
sehemu ya mpango wa hoteli hiyo kurudisha faida wanayopata kwenye jamii
ili kusaidia kupunguza matatizo na changamoto mbalimbali katika sekta ya
elimu.
“Ni
muhimu kwa wafanyabiashara kushirikiana na jamii inayoitumikia na
tutaendelea kusaidia jamii katika siku za usoni tukiwa kama sehemu ya
jamii husika,’ amesema.
Naye
Mkurugenzi wa Advert Construction Ltd Dhmv Jog amesema kampuni yake
inatambua umuhimu wa sekta ya elimu kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na
taifa kwa ujumla katika kufuta ujinga.
Amesema
kampuni yake kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii kimetoa Tsh
10milioni katika kusaidia kampeni hii ya “Dawati ni Elimu” ili kupunguza
na kuondoa kabisa tatizo la madawati mashuleni Wasanii
wataopata nafasi ya kuonyesha kazi zao za sanaa ya kuchora ni Robin
Mtila, Aggrey Mwasha, Salum Kambi, Cathbert Mkocha, Haji Chilonga,
Tobias Miza, James Haule na Victor Malulu.@michuzi