Header Ads

CHANETA YALIA NA MIKOA KUSHIRIKI TAIFA CUP


CHAMA cha netiboli Tanzania (CHANETA) kimeitaka mikoa mbalimbali ya Tanzania kuthibitisha ushiriki wa mashindano ya Kombe la Taifa ifikapo Desemba 5, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Chaneta Anna Kibira alisema mashindano hayo yatafanyika Desemba 12, kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kibira alisema anatarajia mikoa 29 italeta timu kwenye mashindano hayo ili kuwapa nafasi wachezaji wenye vipaji kuonekana na kuongezwa kwenye akiba ya wachezaji katika timu ya Taifa.

“Uthibitisho uwe mapema, tunataka mikoa itakayoshiriki ihakikishe inatoa taarifa mapema, kwa ajili ya maandalizi,” alisema.

Alisema changamoto kubwa iliyopo mbele yao ni mashindano hayo kutopata udhamini kwa ajili ya kusaidia kufanikisha maandalizi hivyo kuomba kampuni, taasisi na mashirika kujitokeza kuwaunga mkono.

“Tunawaomba wadau wajitokeze katika ufadhili ya mashindano haya muhimu tuweze kufanikisha, angalau kununua maji kwa ajili ya timu zitakazoshiriki na mahitaji mengine muhimu,” alisema Kibira
Powered by Blogger.