DK KAMALA AITAFUTIA PCT SOKO LA PARETO
Hatua
hiyo ni utekelezaji wa diplomasia ya uchumi inayomtaka kila balozi kutafuta
masoko ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Katika
ziara yake aliyofanya katika kiwanda
hicho juzi, Balozi huyo alisema “ nilikuja nchini na wafanyabishara na
wawekezaji 65, wametembelea sehemu mbalimbali za uwekezaji bara na visiwani.”
Alisema
katika utendaji wake kazi za kibalozi nchini Ubelgiji alikutana na kapumi ya
Nilo Vital France/Belgium iliyoonesha nia ya kuendeleza sekta ya kilimo cha
pareto nchini.
“Kampuni
hiyo inataka kufanya biashara na PCT na kwa kuanzia imeahidi kununua tani 40 za
malighafi itokanayo na maua ya pareto kila mwaka,” alisema.
Mbali
na kununua malighafi hiyo, Dk Kamala alisema kampuni hiyo ipo tayari
kushirikiana na kiwanda hicho kuboresha miundombinu ya kiwanda na kutoa misaada
ya kitaalamu na kifedha kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji.
“Hii
ni kampuni kubwa yenye leseni ya kufanya biashara hiyo katika nchi zote za
Ulaya; mkiingia nayo mkataba mtaongeza namba ya masoko, ushindani na hatimaye
faida zaidi,” alisema.
Akimshukuru
balozi huyo kwa kujali maenddeleo ya sekta ya kilimo hicho, Meneja wa PCT,
Martin Oweka alisema aliishauri serikali kurekebisha utaratibu wa utoaji leseni
ya ununuzi wa zao hilo kutoka kila baada ya mwaka mmoja na kuwa kila baada ya
miaka mitano.
Pamoja
na kurekebisha utaratibu huo alisema PCT inapendekeza kampuni zote zenye leseni
ya biashara ya pareto ziwe na utaratibu wa kuingia mikataba ya biashara na
wakulima ili kuwapa uhakika wa soko.
Kwa
mujibu wa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Martin Oweka, Bodi ya Pareto Tanzania
ndiyo yenye jukumu kwa niaba ya serikali ya kutoa leseni hizo.
Akizungumzia
uzalishaji, alisema umeongezeka kutoka tani 50 mwaka 2007 hadi tani 3,000 mwaka
huu.
Alisema
kiasi kilichonunuliwa hakikidhi mahitaji ya kiwanda chao kilichopo mjini
Mafinga chenye uwezo wa kusaga hadi kufikia malighafi dondoo tani 5,000 za maua
ya pareto kwa mwaka.