Mukabwa apania Kuvua Viatu Mashabiki
MWIMBAJI
nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa,
aliyethibitisha kuwa miongoni mwa watakaotumbuiza katika Tamasha la
Krismasi litakalorindima Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia katika
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.
Tamasha
hilo la Krismasi limepangwa kusheheni waimbaji kochokocho wa nyimbo za
Injili, miongoni mwao akiwamo mwimbaji huyo galacha wa nyimbo za Injili,
Mukabwa.
Mukabwa
anatoa mwito kwa watu kujitokeza kwa wingi ili 'wavue viatu' siku hiyo
aliyopania kukonga nyoyo za mashabiki atakapopanda jukwaani katika
tamasha hilo. Kulingana
na taarifa yake iliyotolewa na waandaaji wa tamasha hilo, msanii huyo
amepanga kuwapa mashabiki raha na kuwataka wake mkao wa kula wakisubiri
vitu vyake.
“Nimejipanga,
najua mashabiki wa Tanzania wanataka kitu gani, nitawapa raha, mambo ya
Kuvua Viatu watayasikia na mengine, watafurahi sana. “Kwa vile
Rose (Muhando) atakuwepo, nitashirikiana kwenye wimbo huo na nyimbo
zangu mpya nitazitoa huko kwa mara ya kwanza, ni mambo mazuri
yatakuwepo,” alitamba.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex
Msama alisema Mukabwa aliyeimba kwa kumshirikisha mwimbaji nguli wa
Tanzania, Rose Muhando katika wimbo wa Vua Kiatu, ameahidi kukonga nyoyo
za mashabiki.