Header Ads

WALCOTT AREJEA ARSENAL, POYET ATISHIA KUONDOKA SUNDERLAND, ENRIQUE NJE LIVERPOOL!


ARSENAL_TEAM-INDONESIAPATA HABARI ZA LIGI KUU ENGLAND:
THEO WALCOTT APONA
Theo Walcott anatarajiwa Jumamosi kurejea Uwanjani baada ya kuwa nje kwa Miezi miwili kutokana na kuumia Tumboni ambalo alifanyiwa upasuaji.
Jumamosi, Arsenal inatarajiwa kucheza na Southampton, Klabu ambayo Walcott ndio alitokea, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo itachezwa Uwanja wa Emirates.
Mechi ya mwisho kwa Walcott, mwenye Miaka 24, ilikuwa Septemba 22 dhidi ya Stoke City na ilibidi atolewe nje kwenye Mechi hiyo baada kuumia kwa ndani Tumboni.
Akithibitisha kupona kwa Walcott, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema atamweka Mchezaji hiyo kwenye Kikosi chake cha kuikabili Southampton licha ya Winga huyo kukosa Mechi ya majaribio.
Hivi sasa Arsenal, licha ya kufungwa Bao 1-0 na Mabingwa Manchester United katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi, bado wapo kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 2 mbele ya Liverpool.
GUS POYET ATISIHIA KUONDOKA SUNDERLAND
Gus Poyet, Meneja wa Sunderland, amesema ataondoka Klabuni hapo ikiwa Mkurugenzi wa SokaGUS_POYET wa Klabu hiyo, Roberto De Fanti, atasaini Wachezaji wapya bila ya yeye kuhusishwa.
Poyet, Raia wa Uruguay, alichukua wadhifa wa Meneja wa Sunderland Wiki 6 zilizopita baada ya kutimuliwa Paolo Di Canio na wakati huo alikubali kufanya kazi pamoja na De Fanti na Msaka Vipaji Mkuu Valentino Angeloni ikiwa tu yeye ndio atakuwa Mtu wa mwisho kuidhinisha Mchezaji mpya kusainiwa.
Na sasa Poyet amezungumza: “Tuliongelea hali hii hivi karibuni na kutathmini Wachezaji wanne. Nilichagua wawili. Na mmoja kati ya wawili walioletwa na De Fanti walikuwa hapana. Kama huyo angeletwa, nisingekaa hapa. Mchezaji lazima awe ninaemkubali mimi. Kama sivyo sikubali!”
BEKI LIVERPOOL JOSE ENRIQUE KUPASULIWA GOTI
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema Beki wao Jose Enrique ataikosa Dabi ya Merseyside huko Goodison Park dhidi ya Everton baada kuumia Goti linalohitaji upasuaji.
Enrique, Mchezaji kutoka Spain mwenye Miaka 27, alirejea Uwanjani hapo Novemba 9 walipoifunga Fulham 4-0 baada kukaa nje Mwezi mzima kufuatia maumivu mengine.
++++++++++++++++++++++
Liverpool-Mechi 6 zijazo:
23 Nov: Everton (Ugenini)
01 Dec: Hull (Ugenini)
04 Dec: Norwich (Nyumbani)
07 Dec: West Ham (Nyumbani)
15 Dec: Tottenham (Ugenini)
21 Dec: Cardiff (Nyumbani)
++++++++++++++++++++++
Rodgers alithibitisha kukosekana kwa Jose Enrique alipoandika kwenye Tovuti ya Liverpool na pia kuthibitisha upasuaji huo.
Enrique, ambae alinunuliwa kwa Pauni Milioni 6 kutoka Newcastle Mwezi Agosti 2011, ameanza Mechi 6 za Ligi Msimu huu.
++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi 23 Novemba
1545 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Southampton
1800 Fulham v Swansea City
1800 Hull City v Crystal Palace
1800 Newcastle United v Norwich City
1800 Stoke City v Sunderland
2030 West Ham United v Chelsea
++++++++++++++++++++
Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United
++++++++++++++++++++
Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa
++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
11
12
25
2
Liverpool
11
11
23
3
Southampton
11
10
22
4
Chelsea
11
8
21
5
Man Utd
11
5
20
6
Everton
11
4
20
7
Tottenham
11
3
20
8
Man City
11
16
19
9
Newcastle
11
-1
17
10
West Brom
11
0
14
11
Aston Villa
11
-1
14
12
Hull
11
-5
14
13
Swansea
11
0
12
14
Cardiff
11
-6
12
15
Norwich
11
-12
11
16
West Ham
11
-2
10
17
Stoke
11
-4
10
18
Fulham
11
-9
10
19
Sunderland
11
-14
7
20
Crystal Palace
11
-15
4
Powered by Blogger.