NI WIKIENDI YA DABI ULAYA: MOTO HUKO ENGLAND, GERMANY, RUSSIA, SPAIN, FRANCE…!!
JUU KWENYE CHATI NI DORTMUND v BAYERN, EVERTON v LIVERPOOL!!
WIKIENDI hii Miji ya Liverpool, Moscow,
Seville na Salonika itawaka moto kwa Mechi kali za Dabi ambazo Timu
pinzani za Miji hiyo zitakwaana.
PATA DONDOO ZAKE:
England: Everton FC V Liverpool FC
(Jumamosi Saa 1445 Bongo Taimu)
Klabu hizi zimewahi kutwaa Mataji ya
Ubingwa mara 27 kati yao, Liverpool mara 18 na Everton mara 9, na hivyo
Jiji la Liverpool linabaki ndio Jiji ambalo limetwaa Mataji mengi huko
England likifuatiwa na Manchester, mara 23: Man United mara 20, Man City
mara 3, na kisha London, mara 19.
Hii ni Dabi ya Merseyside ya 221 na
itachezwa Goodison Park, Nyumbani kwa Everton, huku Liverpool wakiwa
Nafasi ya Pili, Pointi 3 mbele ya Everton walio Nafasi ya 6.
Huku Liverpool wakiongozwa na
Mashambulizi ya Mastraika wao, Luis Suárez na Daniel Sturridge, Everton
ni imara mno Msimu huu chini ya Meneja mpya Roberto Martínez ambae
amechukua mikoba ya David Moyes aliehamia Man United.
RUSSIA: PFC CSKA MOSKVA V FC SPARTAK MOSKVA
(Jumamosi Saa 1500 Bongo Taimu)
Valeri Karpin, anaiongoza Spartak
Moscow, ambayo Wiki mbili zilizopita iliitwanga FC Zenit St Petersburg,
ambao ndio Vinara wa Ligi Kuu Russia wakiwa Pointi 3 mbele ya Spartak
Moscow, Bao 4-2.
CSKA Moscow wako Pointi 3 nyuma ya Spartak Moscow na sasa wameanza wimbi la ushinda baada kushinda Mechi 3 mfululizo.
Germany: Borussia Dortmund v FC Bayern München
(Jumamosi Saa 1930 Bongo Taimu)
Mario
Götze, ambae aliihama Borussia Dortmund kwenda Bayern Munich mwanzoni
mwa Msimu, ndie anapamba mtanange huu ambao Mabingwa wa Germany na
Ulaya, Bayern Munich, watatembelea Signal Iduna Park wakiwa hawajafungwa
kwenye Bundesliga Msimu huu.
Bayern, chini ya Pep Guardiola, wapo kileleni mwa Ligi Pointi 4 mbele ya Dortmund inayoongozwa na Kocha Jurgen Klopp.
Greece: PAOK FC v Aris Thessaloniki FC
(Jumapilii Saa 1930 Bongo Taimu)
Aris Thessalinika wanatinga Mechi hii
wakiwa taabani kwani wameshinda Mechi mbili tu za Ligi Msimu huu na wapo
Nafasi ya Pili toka mkiani huku PAOK ikiwa Nafasi ya Pili Pointi 6
nyuma ya Vinara.
Uso kwa Uso, PAOK imeshinda Mechi 48 za Dabi hii dhidi ya 31 za Aris.
Spain: Sevilla FC v Real Betis Balompié
(Jumapili Saa 2200 Usiku Bongo Taimu)
Klabu hizi za Mjini Sevilla, huko Spain,
zinafanya vyema kwenye EUROPA LIGI lakini kwenye La Liga zinasuasua na
Real Betis ndio kabisa kwani wako mkiani.
Msimu uliopita, Real Betis ilinyukwa 5-1 na Sevilla waliokuwa Nyumbani kama itavyokuwa Siku ya Jumapili.
Tangu washinde Mechi yao ya mwisho Mwezi
Septemba walipoifunga Villareal Bao 1-0, Real Betis wamechapwa Mechi 5
za La Liga wakati Sevilla wao hali kidogo shwari kwani katika Mechi yao
ya mwisho waliipiga Espanyol 3-1.
France: FC Nantes v AS Monaco FC
(Jumapili Saa 2200 Usiku Bongo Taimu)
Msimu uliopita Timu hizi zilikuwa Daraja la chini, Ligi 2, na kukutana Mwezi Machi zikigombea Ubingwa wa Daraja hilo.
Msimu huu zipo Ligi 1 na zinafanya vizuri kwa Nantes kuwa Nafasi ya 4 na Monaco Nafasi ya 3.