Header Ads

DANNY WELBECK ATWISHWA ‘ZIGO LA GOLI 20!’

STRAIKA wa Manchester United Danny Welbeck amepewa changamoto ya kufunga Bao 20 na Meneja wa Klabu yake David Moyes ambae amempa lengo hilo Msimu huu.
Welbeck, ambae pia huichezea Timu ya Taifa ya England, Jumamosi alitokea Benchi na kuingizwa Kipindi cha Pili na kufunga Bao pekee na la ushindi wakati Man United inaitungua Norwich City Bao 1-0 Uwanjani Carrow Road kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Hilo lilikuwa Bao la 4 kwa Mechi 5 za Welbeck na huo ulikuwa ushindi wa 4 mfululizo kwenye Ligi kwa Man United.
++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
19
19
42
2
Man City
19
33
41
3
Chelsea
19
16
40
4
Everton
19
13
37
5
Liverpool
19
21
36
6
Man United
19
10
34
7
Tottenham
19
-2
34
8
Newcastle
19
5
33
9
Southampton
19
6
27
++++++++++++++++++++++++
DANNY_WELBECK-30DECHuku wakiwakosa Mastaa wao Majeruhi, Wayne Rooney na Robin van Persie, ingawa wote wanatarajiwa kurejea wakati wowote, jukumu la ufungaji limeshuka kwa Mastraika Javier Hernandez ‘Chicharito’ na Danny Welbeck.
Hali hii imemfanya David Moyes ampe motisha Danny Welbeck, ambae sasa ana Bao 7 kwa Man United na 3 kwa England, kujizatiti ili kupachika Mabao zaidi.
Moyes ameeleza: “Tumemweleza kuwa tunataka kuinua umaliziaji wake. Nadhani atazidisha bidii na atapanda kiwango zaidi. Nadhani Danny ametujibu, sasa anasema: ‘Hii safi, sasa naanza kufunga Magoli na kutambulika!’ Msimu uliopita alifunga Bao 1 na huu ana Bao 7. Ingeweza kuwa vizuri zaidi ya hapo lakini anaelekea kuzuri.”
Moyes aliongeza: “Raundi ya Pili ya Msimu inakuja, hakika lazima atazame kufunga Bao 20. Tunataka yeye afanye hivyo wakati hatuna Wayne, hatuna Robin, tunataka Watu wachukue jukumu.”
Wachambuzi wanahisi Msimu huu Danny Welbeck amekuwa akifunga sana kwa sababu tu Moyes mara nyingi humchezesha kama Straika wa kati tofauti na Msimu uliopita, chini ya Sir Alex Ferguson, ambae alipenda sana kumutumia pembeni kwenye Winga, na hasa kushoto, na kumtaka  kushambulia kwa kutumbukia katikati.
MAN UNITED-MECHI ZIJAZO:
Jan 1, Saa 2030: Man Utd V Tottenham [LIGI KUU ENGLAND]
Jan 5, 1930: Man Utd V Swansea [FA CUP-Raundi ya Tatu]
Jan 7, 2245: Sunderland v Man Utd [CAPITAL ONE CUP-Nusu Fainali, Mechi ya 1]
Jan 11, 2030: Man Utd V Swansea [LIGI KUU ENGLAND]
Jan 19, 1900: Chelsea V Man Utd [LIGI KUU ENGLAND]
Jan 22, 2245: Man Utd V Sunderland [CAPITAL ONE CUP-Nusu Fainali, Mechi ya 2]
Jan 28, 2245: Man Utd V Cardiff [LIGI KUU ENGLAND]
Powered by Blogger.