Header Ads

MOURINHO: ‘SUAREZ ANAJIRUSHA KAMA YUPO BWAWA LA KUOGELEA!’

>>‘KOSA PEKEE LA REFA HOWARD WEBB NI KUTOMPA KADI SUAREZ!!’
>>BRENDAN RODGERS: “ILIPASWA ETO'O APEWE KADI NYEKUNDU!
SUAREZ_v_ETOOMENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amesema Straika wa Liverpool Luis Suarez alipaswa kupewa Kadi za Njano kwa kujiangusha kwenye Mechi ya Jana Usiku Uwanjani Stamford Bridge ambayo Chelsea iliitwanga Liverpool Bao 2-1.
Katika moja ya matukio ya Suarez ni pale alipokuwa akimfukuza Cesar Azpilicueta ndani ya Boksi na kugongana na Samuel Eto'o na hilo limemkera Jose Mourinho aliesema: “Hakuzongwa. Suarez alizidiwa maarifa na Azpilicueta ambae alikuwa na Mpira huku akitoka nje ya Boksi. Suarez akaamua kujirusha kama vile anadaivu kwenye Bwawa la Kuogelea!”
Mourinho aliongeza: “Ni mjanja kwani anajua yuko kwenye Boksi na nyuma ya Goli wapo Mashabiki wa Liverpool! Lakini Refa Howard Webb alikuwa Mita 10 tu na nadhani kosa pekee alilofanya ni kutompa Kadi ya Njano Suarez!”
Tukio hilo lilitokea katika Dakika za mwisho za Mechi ambayo Liverpool walitangulia kufunga kwa Bao la Martin Skrtel na Chelsea kujibu kwa Bao za Eden Hazard na Samuel Eto'o.
Pia Mourinho alieleza: “Siku zote nafurahi kumuona Suarez kwani ana Kipaji, anajituma na ana ari ya ushindi. Ni Mchezaji Bora. Lakini Nchi hii ni spesho. Mimi si Muingereza lakini nina wajibu kutetea thamani ya Soka hapa. Kitu kimoja bora tunacho hapa ni kuwa Watu hawapendi kuhadaa. Ile hali iliyokuwepo kati ya yeye na Azpilicueta na Eto'o ni lazima ikome au apewe Kadi za Njano kwani si kitu chema kwa Soka letu.”
Suarez, ambae ni Raia wa Uruguay, Msimu huu amefunga Bao 19 katika Mechi 14 tangu arejee Kiwanjani akitokea kwenye Kifungo cha Mechi 10 kwa kumuuma Meno Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, Mwezi Aprili kwenye Mechi kati ya Liverpool na Chelsea.
Brendan Rodgers atetea!
Hata hivyo, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, ambae alikuwa Msaidizi wa Jose Mourinho kati ya Miaka 2004 na 2007 wakati wa himaya ya kwanza ya Mourinho huko Chelsea kwa mara ya kwanza, alikuwa na mtazamo tofauti na hasa tukio la Eto’o kumchezea faulo Jordan Henderson iliyoleta Frikiki iliyozaa Bao la Skrtel.
Rodgers amedai: “Ilipaswa Eto'o apewe Kadi Nyekundu! Najua tumefunga kwa faulo yake lakini ile ni rafu mbaya na hakupata hata Kadi ya Njano!”
Kuhusu Suarez, Brendan Rodgers ameeleza: “Luis Siku zote atasababisha Mabeki wamvae, ndio maana yuko kiwango cha juu Duniani. Kitu ambacho hakutegemea ni kugongwa na Mtu ambae hana Mpira. Pale alikuwa akikimbia kumkabili Azpilicueta na Eto'o ana ujanja wa Mtaani, alifanya safi, alimziba Suarez. Siku nyingine unaweza kutoa ile iwe Penati kwa sababu amemzuia!”
Brendan Rodgers alimalizia: “Ni dhahiri, Mourinho atamtetea Mchezaji wake na mimi nitamtetea wangu!”
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
19
19
42
2
Man City
19
33
41
3
Chelsea
19
16
40
4
Everton
19
13
37
5
Liverpool
19
21
36
6
Man United
19
10
34
7
Tottenham
19
-2
34
8
Newcastle
19
5
33
9
Southampton
19
6
27
10
Hull
19
-1
23
11
Swansea
19
-1
21
12
Stoke
19
-11
21
13
Aston Villa
19
-7
20
14
Norwich
19
-16
19
15
West Brom
19
-5
18
16
Cardiff
19
-15
18
17
Crystal Palace
19
-16
16
18
Fulham
19
-22
16
19
West Ham
19
-10
15
20
Sunderland
19
-17
14
Powered by Blogger.