Header Ads

KIKOSI BORA DUNIANI 2013: MAKIPA 5 WAGOMBEA WATAJWA!


KESHO WAGOMBEA MABEKI KUANIKWA!!
MWAKA JANA WOTE FIFA/FIFPro WORLD XI LA LIGA, MWAKA HUU JE??
fifproILE LISTI YA WAGOMBEAJI KIKOSI BORA DUNIANI imeanza kuundwa baada ya kutolewa Majina Matano ya Makipa watakaogombea kuwemo kwenye Kikosi hicho.
Wagombea 55 watakaochujwa hadi Wachezaji 11 ili kuunda Kikosi Bora Duniani kwa Mwaka 2013, kinachojulikani rasmi kama FIFA/FIFPro World XI, hupatikana kwa Kura za Wachezaji Soka ya Kulipwa Duniani.
FIFA na International Federation of Professional Footballers (FIFPro), yaani Shirikisho la Kimataifa la Wachezaji Soka wa Kulipwa, wamekuwa wakiendesha Kura za Kikosi Bora Duniani cha Mwaka kwa Miaka mitano sasa.
Listi ya Makipa wataowania kuwemo kwenye FIFA/FIFPro World XI ni:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid CF)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea FC)
-Manuel Neuer (Germany, FC Bayern München)
Víctor Valdés (Spain, FC Barcelona).
Majina yatakayofuatia ili kuwemo kwenye Listi ya mwisho ya Wachezaji 55 ni ya Mabeki, Viungo na Fowadi.
Kikosi cha Wachezaji 11 kitatangazwa rasmi hapo Januari 13, Mwaka 2014 huko Zurich, Uswisi kwenye Tafrija maalum ya FIFA Ballon d’Or Gala ambayo pia atatangazwa Mshindi wa FIFA Ballon d’Or, yaani Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2013.
Mwaka 2012, Wachezaji wote 11 walioshinda na kuingia Kikosi Bora Duniani walitokea Spain kwenye La Liga.
++++++++++++++++++++++++++++
KIKOSI BORA DUNIANI 2012:
KIPA: Iker Casillas
MABEKI: Sergio Ramos, Gerard Pique, Daniel Alves, Marcelo
KIUNGO: Xabi Alonso, Xavi, Andrés Iniesta
MAFOWADI: Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao
++++++++++++++++++++++++++++
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio Wachezaji waaoshikilia Rekodi ya kuteuliwa mara nyingi kwenye Kikosi Bora Duniani kwa kuingia mara 6 kila mmoja.
FIFPro tayari imeshatuma Karatasi za Kura 50,000 kwenda Nchi 68 Duniani katika Mabara ya Africa, Asia, Europe na Marekani.
TAREHE MUHIMU KUTANGAZWA MAJINA 55 YA MWISHO:
Desemba 2-Makipa
Desemba 4-Mabeki
Desemba 6-Viungo
Desemba 9-Mafowadi
Powered by Blogger.