WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUJIESHIMU.
Chuo cha uandishi wa Habari na utangazaji Arusha
(A.J.T.C)kinatarajia kufanya maafali yao ya saba hapo kesho kwa wanafunzi wa tasnia ya uandishi wa habari
na utangazaji yatakayo fanyika katika ukumbi wa PPC Arusha.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wanafunzi
ambao wanatarajia kufanya mahafali yao hapo kesho wamesema kuwa wanayofuraha
kwakuwa na hatua kubwa wameipiga kwakuwa mafunzo waliyoyapata kwa kipindi hicho
yameweza kuwaandaa kupambana na
changamoto katika soko la ajira.
Bw Cleopa Mshana na Bi Win Paul wamesema kuwa licha ya kuwa
wao wamesoma mfumo wa zamani wa analogy wanauwezo wa kutumia mfumo mpya wa
Digital kwakuwa wamefundishwa kwa
uchache hivyo kuwataka wanafunzi ambao wanatumia mfumo mpya kupambana nao kwa
unamanufaa katika fani yao.
Pamoja na hayo wahitimu hao wamesema kuwa katika fani yao ya
uandishi wa habari ni fani ambayo inatumika kwa kuwahabarisharisha wananchi na
wala siyo kuwapotosho kama wanavyofanya waandishi waliovamia tasnia hiyo.
Wamewataka waandishi hao wasio na ujuzi wa taaluma hiyo
kufanya mambo ambayo wanayaweza na siyo
kuvamia taaluma hiyo na kufanya waandishi kuonekana ni wapotoshaji kwa uma.
Pia wamesema siku zote waandishi wa habari wanapaswa
kujiheshimu ili kuendana na taaluma yao
waliyo nayo na kujiona wao wamebeba dhamana kubwa kwa jamii kwakuwa wao ni
sauti kwa wasio na sauti.
Chuo hicho ambacho kinatoa taaluma katika fani ya uandishi
wahabari na utangaji na pia kikiwa ni miongoni wa vyuo bora vilivyo hapa nchini
hiyo kesho kitafanaya mahafali yao yakiwa ni ya saba kuwai kufanyika chuo hapo.
Takribani wanafunzi 56 wanatarajiwa kuhitimu hapo kesho
ikiwemo 9katika ngazi ya cheti 47 katika ngazi wa stashahada wote katika tasnia
ya habari na utangazaji ambao wanatarajiwa kuleta mabadiliko katika fani hiyo.
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….