WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KATIKA TASNIA YA HABARI
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Bw Nyerembe Munasa akitoa hotuba yake katika mahaali ya chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha(A.J.T.C) yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS. |
Waandishi wa habari wametakiwa kuuandaa vipindi vyenye
kuelimisha jamii kwakuwa vitaleta
madadiliko ya kimaendeleo na wala siyo
kupotesha na kuvuruga amani ya nchi kwakuwa nitegemeo la nchi na dunia
kiujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw
Nyerembe Munasa katika maafali ya chuo cha uandishi wa Habari na utangazaji
Arusha yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS na kusema niwakati wa
mabadiliko kwa
waandishi hao wa habari waliohitimu hii leo.
\
Pia amewataka waandishi hao kuuandaa vipindi vya mahojiano
ili kuijenga jamii sambamba na kujikita katika kuandika habari za vijijini ambazo
zimefanyiwa uchunguzi kwakuwa ndiko walipo wananchi wasio na sauti.
Pamoja na hayo amewasauri waandishi ambao wamehitimu kuleta
mabadiliko katika tasnia ya habari
nchini kwakuandika na kuandaa vipindi vya makala ambavyo vinahusu maswala
ya rasilimali na utalii uliopo na kuviuza ili
kuondokana na umaskini.
Kwa upande wa Bw Isack Marosek amehimiza waandishi hao
kuhamasisha amani kwakuwa palipo na amani ndipo maendeleo yanapatikana na
upendo.
Jumla ya wahitimu 56 wamehitimu mafunzo yao 9 wakiwa kwa
ngazi ya cheti pamoja na 47 kwa stashahada
ambapo chuo hicho nimiongoni mwa vyuo bora vinavyoongoza nchini kwa
kushika nafasi ya pili.