MAN UNITED WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA LIGI, SPURS NJE LICHA YA ADEBAYOR KUFUNGA
Na BIN ZUBEIRY
KOCHA David Moyes ameendelea kupambana baada ya jana kuiongoza Manchester United kushinda mabao 2-0 dhidi ya Stoke City katika Kombe la Ligi England.
Ushindi huo wa United jana ulitokana na mabao ya Ashley Young dakika ya 61 na Patrice Evra dakika ya 78.
Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City.
Adebayor akishangilia bao lake ambalo hata hivyo halikuweza kuinusuru Spurs na kipigo
Nayo Manchester City iliifunga 3-1 Leicester na kufikisha jumla ya mabao 75 katika mechi 25 za mashindano yote msimu huu.