MAASKOFU ,WACHUNGAJI WABARIKI TAMASHA LA KRISMASI LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA
MAASKOFU ,WACHUNGANJI WABARIKI TAMASHA LA KRISMASI LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA
MAASKOFU
na Wachungaji wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jijini Mwanza,wameunga
mkono Tamasha la Muziki wa Injili, baada ya kuridhia Kwaya ya Makanisa
yao kushiriki tamasha hilo.
Tamasha
hilo la Krismasi la Muziki wa Injili, litafanyika Desemba 25 mwaka
huu,majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Wakizungumza
jana kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha pamoja kati yao na waandaaji
wa tamasha hilo, The Great Lake Zone Entertainment,kilichofanyika
Vizano hoteli, Maaskofu hao walisema, mbali na kutangaza neno la Mungu
na utukufu wake, litasaidaia kuutangaza muziki wa injili wa kwaya za
Makanisa hayo ya Jijini hapa.
“Ni
maono mazuri kwa waandaaji wa tamasha hilo,na sisi Maaskofu tunapaswa
kuwaunga mkono badala ya kuwakatisha tamaa.Haiwezekani tukatafute
waimbaji kuoka Dar es salaam badala ya kutumia hawa tulionao
hapa,”alisema
Askofu
wa Kanisa la Menonite Tanzania (KMT) Nyakato,Albert Randa, alisema
teknolojia imepanuka tofauti na zamani ambapo nyimbo nyingi na nzuri za
kwaya hazikupata fursa ya kurekodiwa.Kwamba ukanda wa Ziwa hasa Mwanza
na Mara kuna waimbaji wazuri wenye vipaji.
Askofu
Charles Sekelwa,alisema jambo hilo (tamasha) likienda vizuri, ni
heshima kwa waandaaji na akawataka Maaskofu wasiwe sehemu ya ubaya bali
uzuri ili sifa na utukufu zimwendee Mungu ikiwa ni pamoja na
kuwahamsisha waumini wao kuja kushiriki tamasha hilo ili kuwaepusha na
starehe zinazomchukiza Mungu.
Hata
hivyo Askofu Sekelwa ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja huo wa Makanisa ya
Kikristo Mwanza, alionya tamasha hilo lisiwe la kisiasa ndani yake, ili
kuepusha maaskofu kuchafuliwa kutokana na kuunga kwao mkono na ushiriki
wao.
Kwa
mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Fabian Fanuel,mgeni rasmi atakuwa
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, na
kutakuwa na chakula cha usiku katika hoteli ya Malaika baada ya tamasha
hilo.
Tamasha
hilo la muziki wa Injili litafanyika uwanja wa CCM Kirumba kuadhimisha
kuzaliwa kwa Masiha (Yesu) kiingilio kitakuwa shilingi 2000 kwa watu
wazima ambapo watoto watalipa shilingi 1000.
Tayari
wasanii na waimbaji maarufu, Martha Mwaipaja ,Nesta Sanga, Neema
Nga’sha,Daniel Safari na mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS)
Pascal Cassian,watanogesha tamasha hilo kwa vibao vyao vilivyotamba na
vinavyotamba kwa sasa katika muziki wa Injili,wamethibitisha kushiriki.
Wengine
watakaopaza sauti zao siku hiyo ni Seiri Andrew (Nzega Tabora), Joseph
Vedasto (Geita), Dan Sanga na Mary Msigwa (Iringa), Pendo Kanyumi,
Christine Victor, Betty Lucas, Excellence Band, Revival Mission Band na
kwaya mbalimbali kutoka Mwanza.